Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Mtoto mwenye ulemavu ana haki ya huduma za kipekee


TKT/UN RADIO/TAS
 Sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010 ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania inafafanua kuhusu neno ulemavu na mtu mwenye ulemavu, Ulemavu ni hali ya kukosa au kushindwa kuwa na fursa ya kushiriki katika maisha ya kawaida ya kijamii kwa kiwango sawa na wengine kwa sababu za kimaumbile, kiakili au sababu za kijamii.

  Mtu mwenye ulemavu ni mtu mwenye udhaifu au upungufu wa viungo, fahamu au akili na ambaye uwezo wake wa utendaji kazi umepungua kutokana na vikwazo vya kimtazamo, kimazingira na kitaasisi.

Mtoto mwenye ulemavu ana haki ya huduma za kipekee na anastahili kupata huduma maalum ya matibabu na nafasi sawa ya elimu na mazoezi pale inapowezekana ili kumsaidia kufikia malengo yake ya maisha.Na pia mtoto mwenye ulemavu ana haki ya kushiriki katika michezo na hawatakiwi kutengwa

  Mapema mwezi March, mwaka huu chama chawatu wenye ualbino mkoa wa Morogoro(TAS) kili andaa semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari namna ya kuandika habari,kuripoti na kuibua fursa za watu wenye ulemavu wakiwemo watoto.

 Kwa upande wake mgeni rasimi  afisa ustawi wa jamii mkoa wa Morogoro Bi, Jeska Kagunila ametoa wito kwa waandishi wa habari na vyombo wanavyo fanyia kazi kuongeza nguvu ya kui elimisha jamii hususani sera na sheria za watoto wenye ulemavu wazifahamu na kuziishi,bi,Kagunila amebainisha idadi ya watu wenye ulemavu mkoa wa Morogoro watu wazima ni 14452 na watoto wakiwa 377.

Aidha mwenyekiti wa TAS Morogoro Nd.Hasani Mikazi amesema semina hiyo ya siku tatu ilifunguliwa tarehe 13 na kuhitimishwa tarehe 15 mwezi huu ukumbi wa Motel 88 Morogoro ilio wajumuisha waandishi wa habari kuminatano kutoka vyombo mbali mbali Radio,Tv,Magazeti na Vya mtandaoni.

 Hata hivyo Mikazi amebainisha kuwa lengo la semina hiyo ni kufungua fursa zinazotolewa na sheria na sera ndani na nje ya mkoa wa Morogoro kwa watoto wenye ulemavu,kwa kuwa wezesha wazitambue,wazijue na kunufaika nazo,kwenye sekta mbali mbali kama Elim,Afya,Uchumi,Mazingira na Michezo.

Post a Comment

0 Comments