Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Uelewa wa maneno ulemavu na watoto wenye ulemavu bado changamoto kwa jamii.


Utofauti wa uelewa kwenye jamii bado nimkubwa kwani hakuna usawa wakutosha kuhusu watoto wenye ulemavu,kila mmoja anaelewa na kupambanua mambo tofauti na mwingine,jambo hili linaonyesha kwamba kunahaja ya mashirika yanayo jihusisha na elimu kwa jamii,serikali na wadau kuongeza jitihada za kuielimisha kuhusu neno ULEMAVU na WATOTO WENYE ULEMAVU.

Kutoka mkoani Morogoro tumewauliza baadhi ya wananchi uelewa wao  kuhusu ULEMAVU na WATOTO WENYE ULEMAVU, Victoria Komba mkazi wa kata ya kingolwira amesema “watoto wenye ulemavu nisawa na watoto wengine kwenye jamii isipokuwa utofauti nikwamba wao utakuta sehemu ya mwili wake unaupungufu wa kufanya baadhi ya mambo sawa na wengine”.

Kwa upande wake Ajeko Mwaipopo mkazi wa kata ya Bigwa manispaa ya Morogoro uelewa wake kuhusu Ulemavu na Watu wenye ulemavu ni mtu mwenye upungufu wa viungo kwenye mwenye mwili wake ambavyo vina sababisha kushindwa kukamilisha majukumu yake mengine kama wengine.

Hata hivyo Pius Edward kutoka kata ya Dumila Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro ameelezea namna anavyo elewa Ulemavu na Watoto wenye Ulemavu, nimtu ambae sehemu ya mwili wake haijakamilika kama walivyo wengine,na ulemavu ni kupungukiwa kiungo au uwezo wa kutekeleza majukumu kwa wakati husika.

Post a Comment

0 Comments