Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

UPUNGUFU WA DAMU SALAMA WACHANGIA VIFO VYA WAJAWAZITO KAGERAUhaba wa damu katika benki ya damu salama mkoani Kagera, yatajwa kuchangia vifo vya Mama na mtoto kutokana na kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.

Hayo yameelezwa na Mratibu wa Huduma ya Mama na Mtoto mkoani Kagera, Neema Kyamba wakati akizungumza na Tanzania Kids Time/UN Radio huku akibainisha kwamba uhitaji wa damu salama kwa wajawazito ni mkubwa hasa wanaojifungua kwa njia ya Upasuaji.

“jamii ijitokeze kuchangia damu salama maana uwezo wetu bado ni mdogo, pia jamii izingatie dalili za hatari kwa wajawazito na kuondokana na imani potofu ili kuokoa maisha ya mama na mtoto wakati wa kujifungua” amesema.

Kaimu Mganga Kuu wa Mkoa wa Kagera Dr, Kiwia Hassan amedai kuwa, kwa miaka mitatu mfululizo mkoa huo haujafikia lengo la ukusanyaji wa damu salama kwa  asilimia 100 ambapo ukusanya huo hufikia asilimia 50 hadi asilimia 60 kwa Mwaka.

“mwaka 2017 tumekusanya unit 9500, mwaka 2018 tumekusanya unit 13,500 na mwaka jana unit 16,000 sasa ili kuendelea ili tupate damu ya kutosha tunaimarisha zile timu za ukusanyaji wa damu salama katika ngazi ya wilaya, vituo  na mkoa” amesema. 

Mratibu Kiongozi wa timu ya Ukusanyaji  damu salama mkoani Kagera Amos Bashweka amesema kuwa,  asilimia kubwa ya wananchi wanashindwa kujitokeza kuchangia damu kwa sababu ya woga huku Taasisi mbalimbali za  Elimu, Dini na Kijeshi ndizo hujitoa kuchangia damu.

Aidha Bashweka amewataka wananchi kuondoa woga na kujitokeza kuchangia damu, kwani wapo wahanga wengi wa ajali, watoto chini ya miaka mitano, na magonjwa mengine yanayohitaji damu Salama hivyo ni  muhimu Damu kupatikana wakati wote katika vituo vya afya.

Na; Rosemary Eliasi- Kagera


Post a Comment

0 Comments