Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Wanafunzi wamehamasishwa kuwania nafasi za uongozi Shuleni ili kujiandaa vyema kulitumikia vyema Taifa Baadae.
Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari wamehamasishwa kuwania nafasi za Uongozi Shuleni ili kujenga kujiamini na uthubutu baadae watakapokua viongozi wa Taifa.

Akitoa ujumbe huo kwa wanafunzi Mbunge wa Viti maalumu jumuiya ya Vyuo vikuu nchini, Daktari JASMINE TIISEKWA katika kongamano la wanawake  lililofanyika katika chuo kikuu Mzumbe kuelekea siku ya wanawake Duniani, amesema wanafunzi wana wajibu wa kutambua badae wanahitajika kulitumikia Taifa katika nafasi mbalimbali za Uongozi.

''Ninyi wanafunzi msiogope kuwania uongozi shuleni namnatakiwa kujiamini kwelikweli maana ndio wategemewa wa Taifa la kesho,wewe usiogope kuwa kiranja wa wenzako shuleni hiyo inakujenga kujiamini''
Akizungumza baada ya maonesho, ISAYA LUPOGO mhadhiri katika chuo kikuu Mzumbe amesema mitaala ya kufundishi shule za msingi na sekondari huzingatia kumjenga mwanafunzi kuwa kiongozi bora na kuwataka wanafunzi kuwa wabunifu katika majuku yao ya uongozi shulei.

ANASTATIAS MDAKU ni mwanafunzi katika shule ya sekondari Mzumbe amesema amejipanga vyema kuwa kiongozi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

''Nimejipanga vizuri kuwania uongozi kwa kufuata taratibu zote zinazokuwepo na pia nawashauri wengine wahamasike kutaka kuwa viranja'' amesema Anastatias.

Nae PATRIK ROBERTY ni mwanafunzi Shule ya Sekondari Mzumbe ambae sio kiongozi shuleni, amesema ni jambo zuri kuwania uongozi shuleni maana humjenga mwanafunzi kuwa imara.

Aidha kongamano hilo la wanawake lilijumuisha wanafunzi wa jinsia zote kutoka Shule za Msingi na Sekondari Mzumbe.

Na, Hamad Rashid Morogoro.

Post a Comment

0 Comments