Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Wanafunzi wenye Ualbino wanatelekezwa Shuleni Wilayani Bukoba.


Wazazi wa watoto wenye ualbino wanaosoma shule ya Msingi Mugeza Mseto iliyopo manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wamelalamikiwa kwa kuwatelekeza watoto wao shuleni.

Mwalimu mkuu shule ya Msingi Mgeza mseto Bi.Joyce Lobozi amesema hayo wakati akizungumza na baadhi ya wazazi wanaoishi wilayani Bukoba wakati wa kikao kilichoandaliwa na chama cha watu wenye ualbino manisaa ya Bukoba kujadili changamoto wanafunzi wenye ualbino.

Amesema kuwa wako baadhi ya watoto waliopelekwa shuleni wakiwa na miaka miwili lakini wamefikia darasa la 5 hadi la 6 bila kutembelewa na wazazi wao na kwamba watoto hao wanakosa upendo wa dhati kutoka kwa wazazi wao na kujiona watofauti na hata baada ya wazazi kupigiwa simu wamekua wakidai hawana nauli.

Medianita Mnanuzi ni mlezi wa wanafunzi shule ya msingi Mugeza mseto amesema kuwa kutokana na kupita kipindi kirefu bila wanafunzi kuwaona wazazi wao, pindi wanapokutanishwa nao huwakataa wakiamini walezi ndio wazazi wao.

Baadhi ya wazazi walioshiriki kikao hicho wameitaka serikali kuwaeliisha wazazi wenye tabia hiyo ili kuondokana na dhana potofu ya unyanyapaa kwa watoto wao na kwamba kwa wanaoshindwa kubadilika wachukuliwe hatua kali za kisheria, kwani hali hiyo humuathiri mototo kisaikolojia.

Katibu wa chama cha watu wenye ualbino Manisaa ya Bukoba Bwana,Frolence Felician ameeleza kuwa, kwa kushirikiana na ofisi za serikali waliko wazazi wa watoto hao wamekuwa wakiwatafuta na kuwapatia Elimu, licha ya kwamba inachukua muda na kwamba wanalo kusudio la kuendelea kukutana na wazazi kuwapa Elimu mara kwa mara.

Na, Rosemary Eliasi-Kagera.

Post a Comment

0 Comments