Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

WANANCHI WAUMIZWA NA GHARAMA ZA MATIBABU BUKOBA

Hositali ya rufaa ya Bukoba mkoani Kagera, imeanza kuwatoza gharama za matibabu wagonjwa walioko kwenye makundi ya msamaha wa matibabu wakiwemo wajawazito na watoto wasiofuata taratibu zilizowekwa na serikali katika upataji wa huduma.

Mganga mfawidhi katika hospitali ya Rufaa ya Bukoba Dr. Mseleta Nyamkoroto amesema hayo wakati akizungumza naTanzania Kids Times/UN Radio,  kufuatia kuwepo kwa malalamiko juu ya wajawazito na watoto wanaofikishwa hospitalini hapo kutozwa gharama za kujifungua na matibabu.

Aidha amesema kuwa, wamefanya hivyo kufuatia baadhi yao kutokufuata utaratibu wa kuanzia kwenye vituo vya chini vya kutolea huduma za afya Kama Zahanati, vituo vya afya na hospitali za kawaida na badala yake wamekuwa wakija moja kwa moja katika hospitali ya Rufaa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi wa hospitali hiyo Pius Ngeze amesema kuwa, wajawazito wengi wamekuwa hawatambui taratibu zinazoelezwa na wizara katika kupata huduma za matibabu.

Hata hivyo baadhi ya wakazi waliozungumza na Kids times wamedai kusikitishwa na suala la kuanzisha gharama hizo bila kutaarifiwa kwani wengine hawawezi kumudu gharama hizo, kwani gharama za anayejifungua kawaida kuwa ni kati ya shilingi 20,000 hadi 40,000 na upasuaji ni kati ya shilingi 50,000 hadi 70,000 na hizo ni gharama za vifaa vinavyotumika.
 
Na,Rosemary Bundala -Kagera.

Post a Comment

0 Comments