Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Wandishi15wanolewa kuandika habari za watu wenye ulemavu wakiwemo watoto


TAS Morogoro.
Chama cha watu wenye ualbino mkoa wa Morogoro (TAS) kwa kushirikiana na shirika la Voice Tanzania wameanza kutekeleza mradi wa “FUNGUA FURSA KWA WATU WENYE ULEMAVU” kwa kuwajengea uwezo wandishi wa habari wa Radio,Tv,Magazeti,Tovuti na Radio mtandao namna ya kuandika na kuripoti habari zinazo wahusu watu wenye ulemmavu wa aina zote wakiwemo Mama na Mtoto.

Mafunzo hayo ya siku tatu(3) yameanza March,13-March15 mwaka huu katika ukumbi wa  Motel 88 iliopo mkoani Morogoro yanayo husisha waandishi wa habari kumi natano(15),lengo kuu likiwa ni kufungua fursa zilizopo kwenye sera na sheria za nchi kwa watu wenye ulemavu. 

Aidha akizungumza katiaka semina hiyo mwenyekiti wa chamahicho Nd.Hasani Mikazi amesema mradi huo utatekelezwa mkoa wa Morogoro na wilaya zake zote, matarajio baada ya mradi ni kuona watoto wana pata Elimu bora,Afya bora na jamii inayobadili mitazamo hasi dhidi ya watoto wenye ulemavu.
TAS Morogoro.

Hata hivyo kwa upande wake mwanasheria Victoria Nyembea amesema sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010 inaeleza kuhusu watoto wenye ulemavu wana haki sawa na watoto wengine wasio na ulemavu, hivyo ana haki ya..
-Haki ya kuishi
-Haki ya kuheshimiwa na kuthaminiwa
-Haki ya kutokubaguliwa
-Haki ya jina na utaifa
-Haki ya kuishi na wazazi wake
-Haki ya kutoa maoni,mawazo na kutoa maamuzi ya ustawi wake.
-Haki ya kulindwa dhidi ya kudhalilishwa kijinsia

Post a Comment

0 Comments