Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

WATOTO ELFU 4238 HAWAJAANDIKISHWA DARASA LA AWALI.Serikali katika wilaya ya KALIUA mkoani TABORA imewataka wazazi ambao bado hawajawapeleka watoto kujiandikisha darasa la awali na la kwanza kuwapeleka kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumza na Tkt Radio Ofisini kwake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya KALIUA, Daktari JOHN PIMA amesema makadilio ya halmashauri kwa mwaka 2020 ni kuandikisha watoto 13,620 wa darasa la awali na watoto 17,887 wa darasa la kwanza huku akibainisha hali ya uandikishaji mpaka sasa kiwilaya.

Aidha Daktari PIMA amesema kupitia kikao cha kamati ya elimu, afya na maji kimewataka watumishi wa umma kusimamia suala la uandikishaji wa watoto kwenye maeneo yao.

 Kwa upande wake BETHOD MAHENGE tarafa ya KASHISHI ameseam wamejipanga kuahakikisha kila mtoto anaandikishwa darasa husikakwani nihaki ya kila mtoto kupata elimu, na kwa upande wa wazazi ambao hawata tii agizo hilo watakuwa wamekiuka makubaliano. 

Hata hivyo wakili DANIEL SALAMBA amewataka wazazi kutii sheria bila shuruti kwa kuwapeleka watoto shule ilisiku ikifika ilio wekwa ya kuandikisha watoto kila mmoja awe amemuandikisha mwanae,kwani vifungu vya sheria vinavyo husu elimu vitaamua vyenyewe kwa mzazi na mtoto mwenye ikiwa kuna uzembe ulio fanywa kati yao. 

Nao baadhi ya wazazi wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu ya umuhimi wa mtoto kwenda shule hasa katika maeneo ya jamii za wafugaji.
 
Simon Jumanne -KALIUA.

Post a Comment

0 Comments