Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

WANANCHI WA MAGENGE WAJITOLEA KUJENGA MADARASA SABA MKOANI GEITA


Wananchi wa kijiji cha Nyamalulu, kata ya Magenge mkoani Geita wamekamilisha ujenzi wa vyumba saba vya madarasa ya shule ya msingi Mbegete ili kupunguza adha kwa watoto wao wa kutembea umbali mrefu.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari wamesema, kilichowasukuma zaidi kujenga madarasa hayo ni kutokana umbali wa shule mama ya Nyamalulu hali ambayo inapelekea watoto wengi kuishia njiani.

 Deus Kaboja ni Mwenyekiti wa mtaa wa izenga basumba ambapo shule ya msingi ya Mbegete imejengwa, ameeleza kwamba mbali na kukamilika kwa ujenzi huu bado wanachangamoto ya kuwahamasisha wananchi kwani baadhi yao waligomea shughuli hiyo.

“watu wengine walishindwa kuitikia wito wa uchangiaji, ikabidi tuanze kutumia kuvu ya ziada ili tukalimishe ujenzi na watoto waweze kusoma” ameeleza.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Magenge Edward Misungwi, amesema kuwa, shule hiyo ina wanafunzi mia nne, walimu wanne na wanatarajia kujenga nyumba za walimu katika shule hiyo.

“tunampango wa kujenga nyumba za waalimu ili watoto wapate huduma nzuri, hivyo wananchi waendee kujitolea ili kukamilisha ujenzi”
 
Na; Nicholas Paul –Geita

Post a Comment

0 Comments