Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

WATOTO WENYE ULEMAVU WAPEWA MSAADA NJOMBE

Zaidi ya shilingi laki saba ambazo Ni michango ya wananchi wa Mjimwema Mkoani Njombe, zimekabidhiwa kwa Maria Mtitu mama mwenye watoto wawili wenye Ulemavu wa akili.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada  huo Mratibu  wa  kampeni ya  TUNAISHI  NAO  inayoendeshwa  na kituo cha radio mkoani humo  Fikirini Ngairo, amewapongeza  wananchi  kwa  kushiriki kikamilifu  kuchangia  fedha  hizo  zitakazo msaidia  Bi. Maria kuhudumia na kununulia mahitaji ya  watoto  hao.

“Wananchi  wa  Mtaa  wa  Mjimwema  wamechangia  shilingi  laki  tatu  na  elfu  21  na  mia  mbili  na  kufanya  jumla  ya  shilingi  laki  saba  na  elfu  ishilini  na  moja  na  mia  mbili  ambazo  zimekabidhiwa  kwa  mama  huyo  mwenye  watoto  wenye  ulemavu  wa mtindio  wa  ubongo” amesema.

Baadhi ya  viongozi  wa  serikali  wa  mtaa  wa  Mjimwema  akiwemo  Afisa Mtendaji  Elia  Chilatu  amesema  watawaunganisha  watoto  hao  na  Afisa  elimu  kata  ya  Mjimwema  ili  kuwapeleka kwenye  shule  zinazolea  watoto wenye mahitaji  maalumu ili wasomeshwe.

“Afisa Elimu wa kata ameniambia nipeleke majina lakini wao watawatafutia shule hawa watoto watakapofanikisha utaratibu wao” amesema. 

Pia Mama wa watoto hao  wawili ambao wanaumri wa miaka 7 na 10 Maria  Mtitu, ameshukuru kwa  msaada  huo  uliotolewa  na  wananchi   na kwamba  itamsaidia  kutatua  changamoto  zilizokuwa  zikimkabili.

Na; Marco Kilangwa- Njombe

Post a Comment

0 Comments