Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Asilimia 94 ya watoto wanaotumikishwa wako kwenye kilimo, misitu na uvuvi-ILO Tanzania

June,12 ya kila mwaka ni siku ya kupinga utumikishwaji wa watoto, mwaka huu ikiadhimishwa katikati ya  jinamizi kubwa la virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19. 
 Meneja Miradi wa shirika la kazi duniani ILO Tanzania, Dkt. Gerson Nyadzi amesema hali ya utumikishaji watoto asilimia kubwa iko kwenye sekta ya kilimo,Misitu na Uvuvi.

Amebainisha hayo wakati akihojiwa na kituo hiki cha TKT/UN RADIO kuhusu siku ya kupinga utumikishawaji watoto duniani.

Aidha Dkt Nyadzi anabainisha changamoto wanazokumbana nazo kuhusu utumikishwaji wa watoto nijinsi ya kuwabaini watoto wanao fanyishwa kazi chini ya miaka 18 jamii imekuwa naushirikiano hafifu wakati mwingine,hukuwengi wao wakisema nimwana familia na anafundishwa kazi, jambo ambalo sio sahihi.

Post a Comment

0 Comments