Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

CORONA ISIWE CHANZO CHA KUPOTEZA NDOTO ZA WATOTO


KUFUATUA kuwepo kwa likizo ndefu ya COVID 19, kwa wanafunzi nchini, jamii imekumbushwa kuendelea kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya Ukatili na kuepusha mimba za utotoni ili kujenga Tanzania yenye maadili, maendeleo na kuifikia Tanzania ya Viwanda. 

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Taasisi ya kutetea haki za Wanawake na watoto kupitia Vyombo vya habari, Bi. Rose Reuben baada ya kuzungumza na TKT/ UN ambapo amesema kuwa wazazi na walezi wanapaswa kuwaelekeza watoto wao katika kucheza michezo yenye maadili, na kuwasimamia katika kujisomea kipindi hiki cha likizo iliyotokana na janaga la Ugonjwa wa homa ya Mapafu nchini.

“kwa mujibu wa tafiti nyingi zilizopita zinaonyesha kuwa unyanyasaji mwingi wa watoto unafanywa na watu waliokaribu nao hivyo tunaikumbusha jamii kipindi hiki cha Corona watoto wapewe nafasi ya kujieleza, wapate malezi bora na kufichua unyanyasaji wa kijinsia unapotokea, kwani serikali yenu pamoja na shirika la UNICEF waliweka agenda ya Malezi ya watoto Mwaka 2016 na 2019 hivyo wazazi angalieni majukumu yenu kwa watoto isiwe bora malezi bali yawe Malezi bora kwa watoto” amesema.

Pia Bi. Rose Reuben ameonya wanafunzi kutoitumia likizo hiyo katika kujiunga kwenye mambo yasiyofaa na yasiyoipendeza jamii bali watulie nyumbani pamoja na kutoa taarifa kipindi wanapotishiwa baada na kabla ya kufanyiwa ukatili wa aina yoyote katika jamii, huku wazazi wakitakiwa kuepusha ndoa na mimba za utotoni kwa watoto wao.

“kuwepo kwa janga la Corona isiwe chanzo cha kukatisha ndoto za wanafunzi hivyo tunaiasa jamii katika janaga hili wasiongeze janga lingine la kuongeza ndoa na mimba za utotoni, ulawiti na ubakaji kwa watoto hivyo ni jukumu la kila mzazi na mlezi kipindi hiki watoto wanalindwa hadi pale shule zitakapofunguliwa” amesema Bi. Rose 

Katika hatua nyingine, Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mkoani Morogoro Siriel Mchembe akizungumza na TKT/ UN amepiga marufuku kwa wananchi ambao wanamaliza kesi za mimba za utotoni nyuma ya pazia, kwani Sheria itachukua mkondo wake, huku akisisitiza suala hilo kuwa agenda katika vikao vyote vya kata na vijiji ili kuweza kutokomeza mimba za utotoni wilayani humo.

"Mtu anakamatwa amempa mimba mtoto wa shule, watu wanamaliza suala hilo kimya kimya unasahau kuwa yule mtoto amepotezewa maisha yake, naomba tujirekebishe wale wote wanaofanya hivyo kwani wilaya ya Gairo inaongoza kwa uharifu huu wa mimba za utotoni ...Mimi ninauita uhalifu, wananchi waache kuwaficha hao wanaowapa mimba Watoto" amesema Siriel.

MOROGORO
NA, SHUA NDEREKA

Post a Comment

0 Comments