Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Tuna wafunga jumla liwefundisho, wanaowapa mimba na kukeketa watoto wakike.

 Mkuu wa wilaya ya Gairo Mh.Siriel Mchembe atangaza kiama kwa wazazi na walezi wanao ozesha na kuwakeketa watoto wakike,kwani jambo hilo niukiukwaji wa haki za binadamu na lina zohofisha kufikia malengo endelevu ya kudumu ya umoja wa mataifa ifikapo mwaka ,2030 hususani lengo namba nne(4) lakupata elimu bora kwa kila mtu,SDGs.

Mh.Mchembe amebainisha hayo wakati wa mahojiano  maalumu ya siku ya mtoto wa afrika na TKT/UN RADIO mapema hii leo,ambapo amesema wilaya ya Gairo ina watu wengi jamii ya kifugaji na kabila la wakamba ndio wanao endelea kuozesha nakuwakeketa watoto wakike kwa usili mkubwa.

Aidha amekili kuwepo kwa matukio ya mimba za utotoni na kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na ndugu ,rafiki wakaribu,hivyo mtoto anapo pata ujauzito hatajwi muhusika wa ujauzito huo nakusababisha kamati ya ulinzi na usalama kushindwa kupata ushahidi dhidi ya hatua zingine za kisheria.

Katika hatua nyingine Bi,Mchembe amewaonya shangazi wa watoto wakike kuendelea kukiuka maagizo ya serikali kuto wafanyia vitendo vya ukeketaji watoto wao,na akawakumbusha sikuhii muhimu ya maadhimisho ya mtoto wa afrika kuwa siku muhimu kwa watoto kutafakari haki na wajibu wao kwa familia na taifa kwa ujumla ilikuunga mkono juhudi za serikali kuleta maendeleo ya nchi.

Post a Comment

1 Comments