Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Matukio ya vifo vya watoto mkoani njombe

  Jeshi la polisi mkoa  wa Njombe limethibitisha kumkamata daktari wa hospitali ya Ikonda Dkt Mabula Pascal ambaye ni dereva wa gari lililowagonga watoto wawili wa kijiji cha Ng'anda  hapo jana.

Aidha Kamanda wa  jeshi la polisi  mkoa  wa  Njombe Hamis  Issa  amesema chanzo cha tukio hilo ni ulevi wa pombe aliokuwa  nao daktari wa hospitali ya Ikonda Wilayani  Makete Mabula Pascal .

Hata hivyo katika  tukio  hilo lililotokea kijiji  cha Ng'anda  kata ya Makoga limesababisha  kifo cha  mwanafunzi  anayesoma kidato cha kwanza katika shule ya  sekondari  Makoga  Enieth  Mligo   na  majeruhi Tukuzeni Mgeyekwa  wa darasa la saba  anaeendelea na matibabu kituo  cha  afya  Makoga.

Katika  hatua  nyingine  kamanda  wa  polisi  mkoa  wa  njombe  Hamis  Issa  amesema mtoto mwingine  mwenye umri wa miaka minne amefariki  kwa  kugonjwa  na gari aina ya canter  mjini  Makambako majira ya saa mbili  usiku katika  barabara kuu  ya  Iringa Mbeya.

Kamanda  Issa pia amesema jeshi  la  polisi  linamshikilia  mzazi  mmoja  wa  Matiganjora  kwa tuhuma za kumuua  mtoto  Jesca  Jairo mwenye umri wa miaka  mitano  aliyekutwa  amefariki kando  ya  nyumba  yao kwenye miti ya paina.

Post a Comment

0 Comments