Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Wafungwa wengi walio fungwa gereza la njombe wana makosa ya mauwaji ya watoto


Wananchi  Wilayani  Njombe  wametakiwa  kuacha  tabia  ya Ukatili ikiwemo mauaji dhidi  ya  watoto  ambayo  yameendelea kujitokeza kwa baadhi ya maeneo Wilayani humo.

Rai hiyo imetolewa  na mkuu wa  Wilaya  ya  Njombe Bi Luth  Msafiri akiwa katika kijiji cha Matiganjora kufuatia mama mmoja  kutuhumiwa kumuua mtoto mwenye umri wa miaka 5 aliyekuwa anaishi nae.

Katibu tawala Wilaya  ya  Njombe  Emmanuel  Geoge  ameshauri  wananchi  kutoa  taarifa  za  matukio ya  uharifu yanapotokea na kutaka kuacha tabia  ya mauaji.

Msaidizi  wa  magereza  Wilaya  ya  Njombe ASP Elioth Kingu amesema idadi kubwa  ya wafungwa waliopo Njombe ni wafungwa wa mauaji  ya watoto,huku Mkuu wa  upelelezi Wilaya  ya  Njombe ASP  Augustino  Ndamgoba akisema mauaji  mengi yanafanyika baina ya ndugu wenyewe.

Msemaji  wa familia  ya  Jairo Mkanga Bwana  Keneth  Nyagawa  akaeleza  namna tukio lilivyotokea  hadi  mama wa kufikia kumfanyia  ukatili wa mauaji  mtoto wa mme wake kwa kumnyonga na kamba  shingoni. 

Nao  wananchi  wa  kijiji  cha  Matiganjora  wakiongozwa  na mwenyekiti Bi. Grace Nyagawa   wanaungana  na  serikali  kukemea  vikali  tabia  za mauaji  ya  watoto na kutaka  serikali kuchukua hatua  kali dhidi ya matukio wakiwemo wauwaji.

Hivi karibuni jeshi la polisi limemshikilia mama mmoja  wa kijiji  cha  Matiganjora kata ya Ikuna Wilayani Njombe kwa tuhuma za mauaji ya mtoto.


Na,Michael Ngilangwa.

Post a Comment

0 Comments