Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

HOME START YATOA MAFUNZO KWA WAHUDUMU NGAZI JAMII MOROGORO.

 


Asasi ya kujitolea ya Home Start inayofanya kazi ya kutoa huduma kwa Familia Changa zenye changamoto za malezi ya watoto ambao hawajafikia Umri wa kusoma, imetoa mafunzo kwa wahudumu 12 ngazi ya jamii Manispaa ya Morogoro tayari kuanza kazi ili kutengeneza usawa wa Maisha na malezi Bora ngazi ya Familia.

Wahudumu hao wa familia waliopewa mafunzo katika ukumbi wa Kilimo Manispaa ya Morogoro, watafanya kazi ya kusimamia Famili mbili kwa kila mmoja ndani ya Mwaka mzima huku wakizitolea taarifa kwa mratibu wa Asasi, ambaye ataziwasilisha taarifa hizo kwenye Ofisi ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro.

Akizindua Mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Home Start Tanzania Bi, ANNA TEMBA pamoja na mambo mengine pia ameiomba Serikali pamoja na wadau kutoa ushirikiano kwa wahudumu walio pewa mafunzo ili kuzisaidia Familia zenye changamoto ya Malezi.

 ‘’Hawa wahudumu tuliowapatia mafunzo tunaamini wataenda kuleta mabadiliko kwenye ngazi za familia, mimi kama Mkurugenzi wa Home Start naiomba Serikali na wadau kuweza kuwapa ushirikiano ili kuifanikisha vema kazi ya kusaidia Familia’’ alisema Anna Temba

VIPAUMBELE.

‘’kwa kweli kipaumbele kikubwa kwa Home Start tulichonacho ni Mtoto kwanza, tunatamani kuona kila mhudumu kujua haki zote za mtoto na kuhakikisha jamii inazifahamu na kumlinda Mtoto ipasavyo’’Anna.

LENGO LA ASASI.

Kaimu mratibu wa Home start Manispaa ya Morogoro, Delfina Thomas Pacho alisema ‘’Asasi yetu ya Home Start inafanya kazi kwenye jamii kuziepusha Familia kusambaratika kutumia wahudumu walezi ambao wana uzoefu wa malezi ya Familia na waliopokea mafunzo maalumu ya namna ya kuzisaidia familia zenye changamoto ya malezi’’

Aidha Asasi hiyo ilianza Mwaka 2009 Nchini Tanzania hadi sasa imezisaidia Kaya zaidi ya 520 katika kuboresha malezi sahii ya watoto na kutatua Migogoro ya Familia.

Miongoni mwa waliopokea mafunzo ni Sineno Faida na Anna William walizungumza kwa niamba ya wenzao‘’katika mafunzo yetu ya leo nimejifundisha katika Familia suala zima la malezi anatakiwa ahusike Baba na Mama kwahiyo wote wawili wanatakiwa waisikie changamoto ya Mtoto na wampee nafasi ya kumsikiliza na kuitatua changamoto ya Mtoto wao‘’ Sineno Faida.

Na, Anna William akasema ‘’ yani mimi katika mafunzo ya leo nilichojifunza ni namna ya kuisaidia Jamii katika kutatua migogoro na kutumia fursa zilizopo katika Jamii’’

Hata hivyo miongoni mwa mada zilizofundishwa katika mafunzo hayo ni pamoja na wahudumu ngazi ya jamii kutambua haki za watoto, wajibu wa muhudumu anayejitolea kwa Familia pamoja na kufanya tathmini baada ya kuisaidia Familia.

 

Post a Comment

0 Comments