Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

TAKWIMU: ZAIDI YA BILIONI 10 ZILITENGWA KUNUNUA CHANJO ZA WATOTO NCHINI

 

                                           Picha na eatv.

Kwa mujibu wa Hotuba ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto ya Mwaka 2020/2021, katika kipengele C cha utekelezaji wa majukumu ya idara kuu ya afya (fungu 52) huduma za Chanjo.

 Jumla ya watoto 8,082,861 walipata chanjo ili kuzuia ugonjwa wa surua na rubella, sawa na asilimia 112% iliyovuka lengo la kutoa Chanjo kwa watoto 7,216,840 na watoto 4,040,654 sawa na asilimia 114% ya lengo la watoto 3,544,433 walipata chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kupooza kwa nchi nzima, kwanzia Mwezi Julai 2019 hadi kufikia Machi 2020.

 Jedwali hapa chini linaonesha watoto waliokusudiwa na waliofikiwa kupatiwa Chanjo ya Surua, Rubella na ugonjwa wa kupooza sambamba na aina nyingine za Chanjo zilizonunuliwa na Serikali kwa kipindi cha Mwaka 2019/2020.

 

AINA YA CHANJO

WATOTOWALIOKUSUDIWA KUAPATA CHANJO.

WATOTO WALIOPATA CHANJO.

 

ASILIMIA

Surua na Rubella,

7,216,840

8,082,861

112%

Kupooza

3,544,433

4,040,654

114%

 

AINA NYINGINE ZA CHANZO ZILIZONUNULIWA 2019/2020.

 

AINA YA CHANJO

AINA YA UGONJWA.

IDADI YA DOZI.

BCG

Kifua Kikuu

2,000,000

bOPV

Magonjwa ya kupooza

2,000,000

TT

Pepopunda

2,000,000

PCV13

Nimonia na Uti wa mgongo

3,520,600

Rota

kuhara

4,237,800

HPV

saratani ya mlango wa kizazi

580,000

IPV

kupooza kwa watoto.

6,232,800

Penta

Dondakoo, Kifaduro, Kupooza, homa ya ini na homa ya uti wa mgongo.

 

4,048,850

Chanzo: Hotuba ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto ya Mwaka 2020/2021.

Waandishi wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: -

John Kabambala: kabambalajohn@gmail.com na

Hamad Rashid: hamadrashidhd@gmail.com

Post a Comment

0 Comments