Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

TAKWIMU: WILAYA YA KAKONKO INA KIWANGO KIKUBWA CHA MAAMBUKIZI YA MARALIA NCHINI

 


Kwa mujibu wa Ripoti ya Atlasi ya Malaria ngazi ya Halmshauri iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),  Mwezi Agosti 2018 inaenesha, Kiwango cha juu cha maambukizi ya Malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano ni asilimia 30.8 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko na kiwango cha chini kipo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma ambayo ni asilimia 14.7. kwa Mwaka 2017. 

Aidha Mkoa wa Kigoma una kiwango cha juu zaidi kuliko mikoa yote nchini katika maambukizi ya malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano ikiwa ni asilimia 24.4, kiwango hiki cha maambukizi ni kikubwa zaidi ya mara tatu ukilinganisha na wastani wa kitaifa asilimia wa Asilimia 7.3.

 

Jedwali hapo chini linaonesha asilimia za maambukizi ya Malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kwa Halmashauri za Mkoa wa Kigoma.

 

MKOA

HALMASHAURI

ASILIMIA YA KIWANGO CHA MALARIA

 

 

 

KIGOMA

KAKONKO

30.8%

KASULU

27.6%

KIBONDO

25.8%

KIGOMA

25.1%

BUHINGWE

24%

KASULU MJI

15.4%

KIGOMA MANISPAA

14.7%

Chanzo: NBS

Waandishi wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: -

John Kabambala: kabambalajohn@gmail.com

Hamad Rashid: hamadrashidhd@gmail.com

Post a Comment

0 Comments