Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

TAKWIMU: WILAYA YA ULANGA INAONGOZA KWA MAAMBUKIZI YA MARALIA MKOA WA MOROGORO.

 


 Kiwango cha juu cha maambukizi ya Malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano  katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga  asilimia 17.5%, ilhali kiwango kidogo cha Malaria kipo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ambayo ni asilimia 2.6%, Kwa mujibu wa Ripoti ya Atlasi ya Malaria ngazi ya Halmshauri iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),  Mwezi Agosti 2018. 

Aidha Ripoti ya Atlasi ya Malaria imebanisha, kiwango cha Malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano Mkoa wa Morogoro ni asilimia 9.5%, kiwango hiki cha Malaria ni kikubwa ukilinganisha na wastani wa kitaifa wa asilimia 7.3%. 

Jedwali hapo chini linaonesha asilimia za maambukizi ya Malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kwa Halmashauri za Mkoa wa Morogoro.

 

MKOA

HALMASHAURI.

ASILIMIA         YA KIWANGO CHA MALARIA

 

 

 

MOROGORO

ULANGA

17.5%

MOROGORO

16.2%

MALINYI

13.3%

KILOSA

10.4%

MVOMERO

9.7%

KILOMBERO

8.4%

GAIRO

3.5%

IFAKARA MJI

3.5%

MOROGORO MANISPAA

2.6%

Chanzo: NBS

Waandishi wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: -

John Kabambala: kabambalajohn@gmail.com

Hamad Rashid: hamadrashidhd@gmail.com

 

 

Post a Comment

0 Comments