Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

TAKWIMU VITUO 134 VYA KULELEA WATOTO WADOGO MCHANA VILISAJILIWA NA SERIKALI 2020

 


Mwaka 2020, Serikali ilisajili vituo 134 vya kulelea watoto wadogo mchana ikilinganishwa na vituo 373 mwaka 2019 na kufanya jumla ya vituo vilivyosajiliwa kufikia 1,677. Katika kipindi hicho, jumla ya watoto 163,394 (wavulana 85,175 na wasichana 78,219) waliandikishwa ikilinganishwa na watoto 159,479 (wavulana 82,539 na wasichana 76,940) mwaka 2019, sawa na ongezeko la asilimia 2.5. 

Hili ilitokana na kuongezeka kwa mwamko wa wazazi kuandikisha watoto wadogo kulelewa katika vituo. Aidha, idadi ya walezi wa watoto katika vituo vya kulelea watoto wadogo mchana iliongezeka na kufikia walezi 2,878 mwaka 2020 kutoka walezi 2,563 mwaka 2019. Ongezeko hili linatokana kuongezeka kwa idadi ya vituo vya kulea watoto wadogo mchana. 

Chanzo: Kitabu cha hali ya Uchumi wa Taifa katika Mwaka 2020.

Waandishi wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: -

John Kabambala: kabambalajohn@gmail.com 

Hamad Rashid: hamadrashidhd@gmail.com

 

 

Post a Comment

0 Comments