Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

TAKWIMU ZA WATOTO WALIO KATIKA MKINZANO WA SHERIA

 

 


Kitabu cha hali ya Uchumi wa Taifa cha Mwaka 2020,kinabaisha kuwa Serikali ilitoa huduma za msingi pamoja na huduma za msaada wa kisheria kwa watoto walio katika mkinzano na sheria katika mahabusu za watoto za Mbeya, Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Dar es Salaam. 

Katika kipindi hicho, jumla ya watoto 138 (wasichana 18 na wavulana 120) walio katika mkinzano na sheria walipata huduma za chakula, malazi, mavazi, huduma za matibabu na elimu ikilinganishwa na watoto 250 (wasichana 19 na wavulana 231) mwaka 2019. 

Aidha, jumla ya watoto 78 (wasichana 5 na wavulana 73) waliokuwa katika mkinzano na sheria

walichepushwa kutoka katika mfumo rasmi wa haki jinai kwa kuwarekebisha tabia na kuwaunganisha na familia zao mwaka 2020 ikilinganishwa na watoto 148 (wasichana 59 na wavulana 89) mwaka 2019. 

Watoto walio katika mkinzano na sheria

Mwaka

Wasichana

Wavulana

Jumla

2020

18

120

138

2019

19

231

250

Watoto waliochepushwa (Walio ruhusiwa)

2020

5

73

78

2019

59

89

148

 

 

 

 

Chanzo: Kitabu cha hali ya Uchumi wa Taifa katika Mwaka 2020.

Waandishi wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: -

John Kabambala: kabambalajohn@gmail.com 

Hamad Rashid: hamadrashidhd@gmail.com

 

 

Post a Comment

0 Comments