Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Uongozi wa shule ya msingi GONGONI katika halmashauri ya Manispaa ya TABORA, umeweka mikakati ya kutoa majaribio ya masomo kila wiki ili kuwajengea wanafunzi uwezo kitaaluma na kuongeza ufaulu.Uongozi wa shule ya msingi GONGONI katika halmashauri ya Manispaa ya TABORA, umeweka mikakati ya kutoa majaribio ya masomo kila wiki ili kuwajengea wanafunzi uwezo kitaaluma na kuongeza ufaulu.
 Akizungumza na tanzaniakidstime blog Mwalimu mkuu wa shule ya msingi GONGONI, FELIX GAITAN amesema mikakati hiyo, imesaidia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi ambapo katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana, walishika nafasi ya tano kiwilaya.

Aidha GAITAN amesema mkakati mwingine ni kuhakikisha walimu na wanafunzi wanafika kwa wakati shuleni ili kuendelea na ratiba ya masomo ya kila siku.

Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo, wamesema kwamba mkakati wa kupewa majaribio kila wiki umewasaidia na ikiwa tayari wanaendelea kujipanga kufaulu vizuri katika mitihani ya darasa la saba mwaka huu 2018.

Kwa mujibu wa mwalimu mkuu wa shule ya msingi GONGONI amesema mkakati huo umesaidia shule hiyo mara kwa mara kuwa katika shule kumi bora kiwilaya katika matokeo ya mtihani wa darasa la SABA mwaka 2017. Imetumwa na mwandishi wetu kutoka Tabora.

Post a Comment

0 Comments