Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

wazazi na walezi wanapo wakutanisha watoto katika familia upendo huzidi.


FEB 18, 2018
Wazazi,na walezi wanapaswa kuwakutanisha watoto mara kwa mara  kiundugu, kifamilia,  lengo likiwa ni kufahamiana  ili kuepuka  hali ya kutofahamiana ambapo huweza kutomthaminiana wenyewe kwa wenyewe, au kuoana ndugu kwa ndugu hapo  baadae wanapokuwa wakubwa.
Ushauri huo umetolewa na baadhi ya wazazi  katika halmashauri ya Mji wa Ifakara  Mkoani Morogoro baada ya kuona baadhi ya walezi na wazazi hawakutanishi watoto mara kwa mara ambao ni ndugu kwa muda mrefu, jambo ambalo watoto hushindwa kuwafaham ndugu zao.
Baadhi  ya wazazi akiwemo Buruhani Kilindila na Hadija Mahangila ‘wamesema kuwa ni vyema  wazazi wenzao wawe na tabia ya kukutanisha watoto na kuwatambulisha kwandungu zao  hata kama  hali zao kiuchumi ni mbaya. Hivyo watoto hujenga upendo mzuri wakati wakufahamiana mapema kupitia wazazi.
Aidha wamesema wazazi wenye hali nzuri ya kiuchumi wasiwatenge ndugu zao wenye hali ngumu kwani huweza kuwa chanzo cha kutowakutanisha watoto  wao katika familia zao hata hivyo wakati mzuri wakuwakutanisha niwakati wa likizo kwa wanafunzi na wakati washerehe za mwisho wa mwaka.

Post a Comment

0 Comments