Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Shirika la hacoca mkoani Morogoro limeendelea kutoa elimu kwa wazazi , walezi na vijana kuona umuhimu kwa mama na mtoto katika jamii.


   Shirika la hacoca lililopo ndani  ya halimashauli ya morogoro linalo shughulika na kupinga ukatili wanao fanyiwa wanawake na watoto limeendelea kutoa elimu kwa wazazi , walezi na vijana kuona umuhimu kwa mama na mtoto katika jamii.
  Elimu hiyo imetolewa leo katika viwanja vya shule ya msingi Azimio ikiwa nimuendelezo wasiku ya mwanamke duniani ambayo hufanyika March 8 kila mwaka huku Bi,Sidina Mathias afisa usitawi wajamii ngazi ya halimashauli ya morogoro akiwa mgeni lasimi katika tukio.
   Akizungumza na okoa fm Bi, Sidina amesema nivema jamii kuonyesha ushirikiano kwa wanawake kwa kuwawezesha mitaji na mawazo ilikuijenga Tanzania ya viwanda.
   Hata hivyo Watson Mwankusye  ambae nimsemaji wa ziala katika shirika hilo amesema kuna wanawake wengi na watoto wenye shida katika familia zao hivyo huitataji faraja na matumaini kutoka kwa jamii husika ilikukuza uchumi wa familia.

  Aidha mwalimu mkuu wa shule ya msingi Azimio A  Edith Mkude amesema walimu wana kutana na changamoto nyingi kwa watoto ambazo husababishwa na wazazi kuto elewana ndani ya nyumba jambo linalo sababisha kutofanya vizuri kwenye masomoyao, na Aisha Selemani mwanafunzi wa dalasi la 7  amesema kwamba nibora wazazi kuonyesha upendo na heshima ilikujenga msingi imara katika familia.

Post a Comment

0 Comments