Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Viongozi hao wamezitaja hatua hizo 10 KWENYE MWONGOZO HUO.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF Henrietta H. Fore amesema maziwa ya mama ni muhimu kwa afya ya muda mrefu ya mtoto na hupunguza gharama za matibabu ya afya kwani huepusha magonjwa kama vile kuhara.
Hata hivyo viongozi hao wamesema uamuzi wa mama kumnyonyesha mtoto wake kwa miaka miwili mfululizo unahitaji ushirikiano kutoka ngazi ya familia hadi kitaifa.

Hatua hizo 10 ni pamoja na hospitali kuweka sera ya unyonyeshaji na kuzingatia kanuni za kimataifa za kuwapatia watoto wachanga maziwa ya kopo iwapo inalazimika kufanya hivyo, na serĂ¡ hizo ziwe bayana kwa wahudumu wa afya.
Halikadhalika hospitali zijadiliane na wajawazito na familia zao kuhusu umuhimu wa kunyonyesha mtoto na pia watoto wachanga wasipatiwe kitu kingine chochote zaidi ya maziwa ya mama labda tu ikiwa kuna tatizo la kitabibu.
Mwongozo pia unataka mama aelekezwe athari za matumizi ya kutumia chupa za kunyweshea mtoto maji au maziwa na hata mpira wa kumwekea mtoto mdomoni ili asilie.Taarifa zaidi UN Radio.

Post a Comment

0 Comments