Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

vita nihatari kwa taifa.


Mtoto mmoja raia wa Syria ambaye amekuwa akikimbia vita kwa miaka mitano sasa bado hajaweza kupata unafuu kwa kuwa kila aendako ikiwemo nchini Libya bado hali ni ngumu.
Ni mtoto Bassam mwenye umri wa miaka minane akisema kuwa hawezi kurejea Misrata kwa kuwa kuna vita. Anasema angetaka warejee nchini mwao Syria.Bassam na familia yake akiwemo baba, mama na nduguze walikuwa Misri kwa matibabu wakati vita vinaanza nchini Syria.
Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, familia hii ilihamia Libya kusaka maisha ambako nako hali si shwari.Kila mara milio ya risasi bila kusahau vitendo vya kikatili kutoka kwa makundi yaliyojihami.Baba mzazi wa Bassam, Ali Muhammed anasimulia ukatili alioshuhudia mwanae.
 “Walifunga mwili wa mwanadamu nyuma ya gari na kuuvuta  kupitia barabara kuu na Assam aliona hiyo. Kwa sasa kila mara huamka kutoka usingizini akiwa na uoga.”
Vita na umaskini vimemuathiri mtoto huyo na sasa amekondeana akiwa na uzito wa chini ya kilo 20 huku mwenyewe akikumbuka uzito wake wa awali.Bwana Muhammed anataka wahamie Ulaya akiamini kuwa huko maisha ni bora kuliko Libya hata hivyo wanahofia kuvuka baharí ikizingatiwa taarifa nyingi zinazoonyesha watu wakifa majini. Taarifa hii nikwamjibu wa radio ya umoja wa mataifa.


Post a Comment

0 Comments