Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Zeid aikumbusha Iran, hata akikosa nini mtoto haistahili kunyongwa


Aboklfazi Chezani Sharahi, kwa kosa la kumuua mtu mmoja kwa kumdunga kisu.
Sharahi alikuwa na umri wa miaka 15 tu alipohukumiwa kifo na mahakama moja ya nchini humo, na alinyongwa  Jumatano wikihii.
Zeid Al Hussein amelaani hatua hiyo, akisisitiza kuwa kuwanyonga watoto wahalifu ni ukiukaji wa  sheria za kimataifa  na mtoto hapaswi kunyongwa hata kama amefanya kosa gani.
Sharahi ni  mtoto wa nne kunyongwa nchini Iran tangu tangu kuanza kwa mwaka huuhuku watoto wengine watano walinyongwa mwaka jana.
Hata hivyo amesema kuna taarifa za watoto wengine 85 wanaosubiri kunyongwa na kuongeza ,  “tunaelewa  kuna mtoto mwingine Mohammad Kalhori, hukumu yake ya kunyongwa itatekelezwa wakati wowote lakini naiomba serikali ya Iran kutotekeleza hukumu hiyo na badala yake kuigeuza adhabu ya kifo kuwa kifungo cha maisha.”
Pia kamishna  ameelezea wasiwasi wake  wa kutokuwepo na uwazi kabla ya kutekeleza hukumu ya kifo nchini Iran akisema kwa kutotoa taarifa za wakati wa kutekeleza hukumu hiyo hakuweki rehani tu roho ya mfungwa bali pia kunawaweka roho juu familia na jamaa zake hali inayosababisha msongo wa mawazo.
Zeid amesema ofisi yake iko tayari kuisaidia serikali ya Iran kufuata  wajibu wake kuelekea haki za binadamu na sharia za kimataifa kuhusu haki za watoto hii nikwamjibu wa UN RADIO.

Post a Comment

0 Comments