Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

UNMISS yawanoa Polisi Sudan Kusini kuhusu ulinzi kwa watoto kwenye maeneo yalio na migogoro.


  Sheria ya mtoto ya mwaka 2009 Sura ya 3 kifungu cha kwanza inasema Kumtunza na Kumlinda Mtoto, Sheria hii inasema kwamba Mtoto anahitaji huduma na Ulinzi, Iwapo Mtoto huyu.(a) Niyatima au Ametelekezwa na ndugu zake(b) Ameachwa au anatendwa vibaya na mtu ambae anamtunza na kumlea mtoto au na mlezi au wazazi. Navifungu vingine vinavyoendelea kwenye sheria hii , Jeshi la Polisi  Sudani kusini limeamua kuanzisha mafunzo maalumu kwa maafisa wa jeshi hilo jisigani watamlinda Mtoto kwenye maeneo yote yanayo kabiliwa na migogoro.
Maafisa 23 wa jeshi la polisi la Sudan Kusini wanaohudumu kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini  humo cha UNMISS wamekutana  kwa ajili ya mafunzo maalumu ya kuwalinda watoto katika sehemu za migogoro.Ni wakati wa kujitambulisha mjini Juba kwa maafisa hao walio na jukumu la kuwalinda watoto. Wametoka sehemu tofauti za Sudan Kusini kwalengo la kujifunza mbinu  bora za  kuwalinda watoto, kama anavyosisitiza kamishna wa polisi wa UNMISS, Bi. Unaisi Lutu Vuniwaqa.
 “  Tunaona umuhimu   wa kuwamulika watoto, hususan waathirika wa makosa ya jinai, watoto kama mashahidi, na watoto kama washukiwa pia. Kuna haja kwetu kupigia debe uimarishaji wa mifumo ya sheria , hasa wakati  huu tunaposhirikiana na  wenzetu hapa polisi wa taifa la Sudan Kusini, kwamba tunahitaji kuendeleza  haki za watoto wanapokabiliana na sheria.”
Darasa limeanza, maafisa hao wa polisi wanajifunza kwa makini jinsi ya kutekeleza kwa vitendo,  elimu na  mbinu wanazopata .  Aja Ndey Begay Mbye ni mmoja wa maafisa hao“Najifunza jinsi ya kukabiliana na watoto, jinsi gani ya kuwahoji, jinsi ya kuwa nao na kuwaonyesha watoto hao mimi ni mama.” Taarifa hii nikwa mjibu wa Radio washirika ya Umoja wa Mataifa UN RADIO.

Post a Comment

0 Comments