Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Agizo kali limetolewa dhidi ya Wazazi na Walezi watakaobainika kutopeleka watoto wao shule au kuwaozesha katika umri mdogo huko wilayani Igunga.
WAZAZI na Walezi watakaobainika kutopeleka watoto wao shule au kuwaozesha katika umri mdogo wilayani Igunga Mkoani Mkoani Tabora watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Agizo hilo limetolewa na Kaimu Katibu Tawala wa wilaya hiyo Shadrack Kalekayo alipokuwa akiongea na wananchi katika kijiji cha Mwakipoleja kilichoko katika kata ya Mbutu wilayani humo.
  Aidhasema hakuna sababu yoyote ile ya msingi inayoweza kumzuia mtoto wa kike au kiume mwenye umri wa kwenda shule asipelekwe kupata elimu kwa sababu serikali imeweka mazingira mazuri ya elimu kwa watoto wote.
  Hata hivyo serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli iliamua kufuta ada na michango yote kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari (kidato cha kwanza hadi cha nne) ili kuwawezesha kupata elimu pasipo kikwazo chochote.
  Nd. Shadrack  dhamira ya serikali ni njema kwa kuwa baadhi ya watoto walikuwa hawapelekwi shule kwa kisingizio cha ada na michangokuzidi, michango na ada zote zimefutwa, pelekeni watoto wenu katika shule za awali, msingi na sekondari, elimu ni bure.

Post a Comment

0 Comments