Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

watoto wametajwa kuwa chanzo cha umaskini na ghasia huko Amerika ya Kusini hayo ya mesemwa na Unicef nchini humo.

Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, Guatemala, Honduras na Mexico ni nchi ambazo kwazo watoto wanalazimika kukimbia ili kuokoa maisha yao. Mary mmoja wa waliorejeshwa anasema..
Hapa kuna ghasia nyingi. Mtu mmoja anafariki dunia kila baada ya siku tatu au nne.Ni hatari sana kutoka nje usiku saa tatu.”
Kijana mwingine kwa jina la Zoe ambaye baba yake alimsaidia kuondoka, akafunguka.
 “Baba yangu alifanya hivi ili kutulinda kwa sababu anapenda maisha yetu yetu yawe bora. Kila baba anatamani hivyo kwa watoto wake. Kwa hiyo nilimwambia nataka kuondoka hapa kwa sababu tunaishi kwenye nchi hatari. Awali ilikuwa tulivu lakini si hivyo tena. Kila unachosikia kila wakati ni mauaji ya vijana kama mimi.”
Akinukuliwa kwenye ripoti hiyo iliyopatiwa jina waliofurushwa Amerika ya Kati na Mexico Mwakilishi wa UNICEF kanda ya Amerika ya Kusini na Karibea Maria Cristina Perceval, amesema vijana wengi wanaorejeshwa nyumbani kutoka Mexico na Marekani hukabiliwa na  unyanyapaa kwa kuwa mipango yao ya kuhamia nje ya nchi haikufaulu.
Halikadhalika ghasia na pia umaskini kwa kuwa huwa wanachukua mikopo kufanikisha safari za nje na kwa kuwa wanarejeshwa hujikuta hawana pa kufikia wala pesa za kujikimu.
  Bi. Perceval amesema ni muhimu kushughulikia hatari zinazopata vijana na watoto hao wanaorejea na kwamba serikali zichukue hatua sahihi.
Mathalani mikakati ya kutatua sababu za kukimbia, kuwapatia watoto huduma muhimu wakati wa harakati za uhamiaji, kuwasaidia na mipango ya kujumuika tena na jamii zao pamoja na kuhakikisha kurejeshwa nyumbani kwa mtoto kunafanyika kwa maslahi yake na si vinginevyo Taarifa hii nikwamjibu wa radio washirika radio ya umoja wa mataia.

Post a Comment

0 Comments