Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Wtoto wakimbizi wa Syria huko Lebanon wapata vyeti vya kuzaliwa kwa urahisi.

Mabadiliko muhimu yaliyofanyika katika utaratibu wa  sheria za Lebanon kuhusu usajili wa watoto umewezesha  zaidi ya watoto  50,000 wakimbizi kutoka  Syria waliozaliwa Lebanon tangu mgogoro uanze  nchini mwao kuweza kusajiliwa.
Kusini mwa Lebanon katika moja ya kambi za wakimbizi wa Syria.
Awali watoto wa wakimbizi wa Syria waliozaliwa nchini Lebanon na kukosa kusajiliwa ndani ya mwaka mmoja baada ya kuzaliwa, walipata taabu kupata cheti cha kuzaliwa.
Wazazi walipaswa kulipa hadi dola 1,500 ili kupata cheti, gharama ambayo ni ya juu na hawakuipatia umuhimu kutokana na mahitaji mengine ya lazima.
Watoto walikosa huduma muhimu kama afya na elimu.
 taarifa hii nikwamjibu wa radio washirika ya umoja wa
Hata hivyo hivi karibuni serikali ya Lebanon ilipitisha uamuzi ya kwamba watoto wote wa Syria waliozaliwa kati ya Januari Mosi 2011 na mwezi Machi 2018 wasajiliwe bila gharama yoyote.
Mohammad Jarjowi, ni afisa wa sheria wa kamati ya kimataifa ya uokozi IRC.
“Sasa tunaweza kutayarisha vyeti vya kuzaliwa na kuvisajili katika masjala ya kigeni hata pale ambapo mtoto alikuwa  amepitisha ukomo wa usajili wa ndani ya mwaka mmoja tangu azaliwe.”
mataifa kutoka New York Marekani.

Post a Comment

0 Comments