Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Profesa wa hisabati ameweza kugundua kipaji cha mtoto mkimbizi kutoka Syria.

Mtoto huyo Abdel Razzaq mwenye umri wa miaka 12 aligunduliwa kipaji hicho na Profesa Abbas Maana  kupitia mradi wa kufundisha watoto unaondeshwa na shirika la kiraia la Teach For Lebanon.
Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Profesa Maana ambaye amekuwa anatembelea nyumbani kwa mtoto Razzaq anasema..
 “Mara ya kwanza nilipokutana na Abdel niliweza kufahamu alikuwa na uelewa mkubwa. Alikuwa na akili, lakini alikosa kujiamini”
 Teach For Lebanon, shirika ambalo linasaidia elimu katika shule nchini Lebanoni tayari limesaidia kuelimisha zaidi ya watoto 5000 wa Lebanon na Syria  ambapo Profesa Maana anasema..
 “Bila kujali utaifa wa mtoto au hali yake ya awali, tunataka kuangazia uwezo wa mtoto na kuongeza uwezo wa stadi alizonazo.”
 Azma hii inaonekana kutimia kwa mtoto Abdel ambaye kipaji chake kingeweza kupotea bila kufahamika Profesa Maana..
 “Nimejifunza kutoka kwa Profesa Abbas maadili mengi ikiwamo kutokata tamaa na kuwasaidia wengine. Ndoto yangu ni kukua na kuwa mwanasayansi kuvumbua dunia inayonizunguka.”
Lebanon inahifadhi watoto wakimbizi waliosajiliwa wapatao 987,000 kutoka Syria ambapo kati  yao hao 490,000 ni watoto wenye umri wa kwenda shule kuanzia umri wa miaka mitatu hadi 18.
UNHCR inasema kuwa watoto wakimbizi 220,000 wanasoma na wenzao wa Lebanon katika shule za umma asubuhi au madarasa ya jioni mahususi kwa watoto wasyria walioko ukimbizi Lebanoni.
 Taarifa hiin nikwa mjibu wa radio washirika UN RADIO.

Post a Comment

0 Comments