Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

MAMA ASIEJULIKANA ATELEKEZA WATOTO WAKE MAPACHA WAWILI (2) WENYE UMRI WA MIAKA MIWILI (2) KITUO CHA MABASI NA KUTOKOMEA KUSIKOJULIKANA.   Jamii wilayani Karagwe mkoani Kagera imesikitishwa na kitendo cha watoto wawili mapacha  wanaokadiliwa kuwa na umri miaka miwili jinsia ya kike kutelekezwa na mama yao  katika stendi ya mji mdogo wa Omurushaka kata ya Bugene wilayani karagwe.

  Akizungumuza na TKT radio katika eneo la tukio lililotokea mapema mwezi huu afisa usitawi wa jamii wilayani Karagwe Owokusima Kahiyura amesema kuwa watoto hao wawili ambao ni mapacha jinsia ya kike wanasadikika kuwa na umri wa miaka miwili na walitelekezwa na mama yao mzazi katika stendi ya magari mji mdogo wa Omurushaka kata ya Bugene wilayani Karagwe kisha mama huyo kutokomea kusikojulikana.

  Aidha baada ya wananchi kubaini kuwa mama huyo ametelekeza watoto hao walitoa taarifa kwa mwenyekiti wa kitongoji cha Omurushaka C kisha naye kutoa taarifa kituo cha polisi Nyakahanga na kubainisha kuwa wao kama ofisi ya usitawi wa jamii watoto hao watawapeleka kituo cha kulelea watoto yatima Ntoma halmashauri ya wilaya Bukoba mkoani Kagera  huku jitihada za mama aliyefanya tukio hilo zikiwa zinaendelea kufanywa ja na jeshi la polisi.

   Hata hivyo tukio hilo ni la pili kuripotiwa kwa kipindi cha mwaka huu  wilayani humo kwani katika kipindi cha mwezi juni mwaka huu  mtoto mmoja alikutwa ametelekezwa  katika shimo la choo mjini Kayanga.
Hata hivyo  nao baadhi ya wananchi akiwemo  Linus Kishenyi na Ashura Ghaibu wamesema kuwa tukio hilo ni la kikatili na kusema kuwa kinachosababisha matukio ya kutelekezwa kwa watoto wilayani  Karagwe ni kutokana na baadhi ya wazazi kuzaa watoto na kuwatupia mzigo wanawake kwa kukwepa majukumu ya kutoa mahitaji ya kulea watoto ni pamoja na wilaya hiyo kuwa mpakani mwa nchi za Rwanda na Burundi kwani baadhi yao hutokea katika nchi hizo  kama wakimbizi ili kutafuta vibarua kutokana na ugumu wa maisha.Na Jovinus  Ezekiel.

Post a Comment

2 Comments

  1. Kinamama wenzangu tujitahidi kuwahurumia watoto tuliowazaa maana sisi ndo wenye uchungu zaidi ya baba zao! Kuna madhara makubwa sana kijamii, kimwili, kisaikolojia na kiroho yanayotokana na kukataliwa kama ambavyo tunawakataa kwa kisingizio cha ugumu wa maisha!?!! ...TUFE NAO!!!

    ReplyDelete