Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Hapa ndipo wanapo somea watoto hawa tangu chekechea hadi walipo mpata msamalia mwema wa wakuunga mkono ujenzi wa jengo moja la darasa, Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora.


Wananchi wanachama wa jumuiya ya ISAWIMA katika wilaya ya KALIUA mkoani TABORA wametakiwa kuacha kuvamia hifadhi hiyo badala yake waitunze kwani ni kichocheo cha maendeleo.
   
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha SHELLA kata ya USENYE kabla ya kukabidhi bandari tatu za bati zenye thamani ya milioni moja na elfu hamsini zilizotolewa na jumuiya ya ISAWIMA ili kuunga mkono ujenzi wa darasa katika shule ya msingi SHELLA mkuu wa wilaya ya KALIUA, ABELI BUSALAMA amewataka wananchi kuacha kuvamia hifadhi hiyo kwani ni mdau wa shughuli za maendeleo.
  
   Awali katibu wa jumuiya ya ISAWIMA, HAMIS SELEMANI amesema ISAWIMA ni mali ya wananchi wanachama kwani mapato yatokanayo na hifadhi hiyo yanalenga kuunga mkono ujenzi wa miundombinu mbali mbali ya kimaendeleo.
Kwa upande wao mkuu wa shule ya msingi SHELLA, ENOCK NTAHOLIJA na afisa elimu kata ya USENYE, DOTTO MDIHU wameishukuru jumuiya ya ISAWIMA kwa kutoa mabati kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu shuleni hapo,  Wazazi na wanafunzi nao wameeleza furaha zao kuhusu upatikanaji wa jingo hilo kwani litawasaidia watoto  wao.
    
  Nae Mwenyekiti wa jumuiya ya ISAWIMA, JAYLANI ADAMU amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuacha kubeza hifadhi hiyo nakuongeza kwa kusema ni vyema wakatoa elimu kwa wananchi kukemea uvamizi ndani ya hifadhi.   Kutoka Wilaya Ya KALIUA, Na Mwandishi wetu Simon Jumanne.
 

 

Post a Comment

0 Comments