Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

VYUMBA (6) KWA WANAFUNZI (1088) hii ni idadi ambayo haiendani na wingi wa wanafunzi waliopo,hiyo staajabu ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi kagera huko mkoani geita ndg.MAHEBE CHIGULU.


    

Serikali imeombwa kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyo jengwa kupitia nguvu za wananchi,ili kuendelea kuwatia moyo wananchi wanaojitolea katika ujenzi katika shule za msingi na sekondari.

   Hayo yamesemwa na Afisa mtendaji wa kijiji cha kagera kata ya ikunguigazi wilaya ya Mbogwe mkoani Geita Ndg.DAUDI SAMANDITO GOMBO wakati akizungumza na TKT Radio,Amesema wamejenga vyumba vinne vya madarasa na serikali ilitakiwa kupaua vyumba hivyo baada ya wananchi kujenga maboma yote.
   Aidha amewaomba wadau wa elimu kujitokeza kutoa misaada ilikuwapunguzia mzigo wananchi wanaojitoa na akaiomba serikali kutochelewa katika ukamilishaji wa vyumba vya madarasa vinavyojengwa kwa kupitia nguvu za wananchi.

  Hata hivyo mwalimu mkuu wa shulehiyo MAHEBE CHIGULU,Amesema shule yake ina wanafunzi 1088 idadi ambayo haiendani na idadi ya vyumba vilivyopo,kwani mahitaji ya vyumba katika shule hiyo ni vyumba 26 na vilivyokamilika ni vyumba 6 tu.

   Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo ndg.PIUS NDULU,Amesema ili kukamilisha vyumba hivyo wao kama kamati wamejipangia kila mwaka wanajenga vyumba vinne vya madarasa kwa kupitia michango ya wananchi.
    Kwa upande wao wananchi wamesema wao walijitoa vya kutosha katika ujenzi wa vyumba hivyo,kutokana na umuhimu wa elimu kwa watoto kwa maisha ya badae.

                              NA NICKIRAUS PAUL LYANKANDO KUTOKA GEITA.

Post a Comment

0 Comments