Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

SHIRIKA LA MOWECS LA IBUA MAKUBWA KATIAKA HALMASHAURI YA MOROGORO LINALO TEKELEZA MRADI WA INUA MTOTO: Shirika lisilo la kiserikali la Morogoro Organization for Women,Elders and Chid Support (MOWECS) linalo shughulika na kuhudumia wanawake,wazee na watoto makao makuu yake yakiwa mkoani Morogoro,limeleta ahuweni kwa wananchi hususanini maeneo liliko anzisha mradi unao wahusu watoto unaoitwa Inua Mtoto.

 Akizungumza na TKT/UN Radio kandoni mwa hafla ya kuuzindua mradi huo katika halmashauri ya Morogoro mkurungezi mtendaji Mery Mafwimbo amesema lengo la kuu la shirika hilo kuwasaidia familia duni, kwa kuwaundia vikundi kasha kuwaombea mikopo ilikuweza kuendesha shughuli wanazo weza kuzifanya wao wenyewe kwenye maeneo yao walipo.

 Aidha Bi,Mery amefafanua kuhusu mradi huo, nikunusuru kundi kubwa la watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu,kupitia wazazi na walezi wao wataweza kunusuru hizo kaya masikini kwa kufanya miradi mdogomidogo ambayo itawasaidia kupata mahitaji muhimu kwenye familia na kuendelea kuwatunza watoto wao,ambapo shirika hilo limefanya utafiti wa awali katika kata tano ndani ya halmashauri ya Morogoro Kihonda,Lukobe,Kichangani,Mkundi na Chamwino wamebaini kuwepo kwa watoto walemavu kumina nne(14),watoto yatima (79) na wale wanao ishi na wazazi wao lakini kwa mazingira magumu familia (150).

 Hata hivyo Afsa maendeleo ya jamii kata ya Mkundi Maria Matandula kwa upande wa serikali amekili kuwepo kwa watoto wengi wanaoshi kwenye mazingira hatarishi katika kata hiyo, nakuongeza kwamba wanakutana na kesi nyingi zinazo wahusu watoto wanao randa randa mitaani na wanapo fuatilia wana gundua wengi kwenye familia zao hakuna malezi shirikishi yanayo wawezesha watoto kuendelea kubaki nyumbani hata kama familia imeyumba kiuchumi.

 Kwabaadhi ya watoto wlionufaika kupewa misaada ya vifaa vya shuleni Zurfa Kasim na Godfray Gabriel wameshukuru shirika hilo kwa kuwapatia dafutari,pencel na pen nakuwaomba waendelee kusaidia watoto wenye mahitaji kamahayo.

 Kwaupande wa wazazi waliohudhuria hafla hiyo wamesema shirika hilo kupitia mradi wake wa Inua Mtoto unaweza kuwa msaada mkubwa kwa jamii hususani kutoa ushari, kurejesha na kuwaunganisha watoto kwenye familia zao kwa wale ambao walisha toroka makwao,kwaupande mwingine Anna Temba amewaomba wazazi na walezi katika familia kuwalea watoto kwa misingi ya kidini kama maandiko matakatifu yanavyo sema mlee mtoto katika njia impasayo nae hataiacha hata atakapo kuwa mzee Mithali 22:6.

Post a Comment

0 Comments