Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

zoezi la kuwarudisha watoto katika familia zao wanaoishi na kufanya kazi mtaani limeanza,hatua hiyo imefikiwa baada ya kugundua ongezeko la watoto 1,254 waishio mitaani.


WIZARA YA AFYA.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amewataka wadau mkoani Mwanza  kushirikiana na serikali kutokomeza kabisa  tatizo la watoto takribani 1,254 wanaoishi na kufanya kazi mitaani jijini humo kwa kutumia mifumo na rasilimali zilizopo kumaliza kabisa tatizo hilo.

Mkuu huyo wa Mkoa pia amesema lengo la kutaka kupunguza tatizo hilo sio la kuwaonea bali pia ni kuwasaidia watoto hao kuondoka na madhara na madhira wayapatayo watoto hao ili waweze kurudi katika familia zao na kuondokana na maisha ya mashaka yanayowakabili.

‘’Unakuta mtoto anakuja mtaani na kupewa msaada unaotosha kwa wiki moja kwa msingi huu mtu huyu anazoea na kujenga tabia ya kutochukia maisha ya namna hii hivyo misaada hii inajenga usugu kwa baadhi ya watu hawa kutoona sababu ya kuachana na tabia ya kurudi au kendelea kuishi mitaani hivyo razima suala misaada liangaliwe upya.’’Alisisitiza Bw. Mongella.

Aidha kiongozi huyo wa Mkoa wa Mwanza ameongeza kuwa mkoa wa mwanza unaweza kutokomeza vitendo hivi kwa kuwa unayo mifumo mizuri ya ufuatiliaji kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa na kuwataka wadau mkoani humo kwa kushirikiana na serikali kuhakikisha  watoto hawa wanarudi katika familia zao na kuwafuatilia kupitia ngazi ya  kijiji hadi mkoa.

Wakati huo huo katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 iko wazi kwani inawataka watoto kuishi na kulelewa katika familia hivyo suala hili linaweza kutokomezwa kwa mjibu wa sheria hiyo.

Aidha Dkt. Jingu ameongeza kuwa watoto hawa lazima warudishwe katika familia zao na uchambuzi ufanyike ili kubaini wale wote ambao hawataweza kurudi katika familia zao basi wapelekwe katika makao ya serikali ya wattoto ili waweze kupatiwa huduma bora ikiwemo chakula na maradhi.

Dkt. Jingu amewataka watoto hao kutambua kuwa wao ni azina ya Taifa hivyo wanatakiwa kuishi katika malezi bora na kuonya kuwa baadhi ya walezi kwa sasa ni waharifu na hivyo kuwafundisha watoto hao uharifu na kujiona wao sio sehemu ya jamii wanamoishi.

Naye Kamishna wa Ustawi wa Jamii hapa Nchini Dkt. Naftali Ngondi wakati akimkaribisha katibu Mkuu katika kikao kazi hicho amsema lengo la kikao kazi hicho ni kuja na mpango mkakati utakaowezesha kufuatilia utekelezaji wa kutokomeza swala la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani kuisha kabisa kwa kuanzia na mkoa wa mwanza.

Aidha Dkt. Ngondi ameongeza kuwa idadi ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani nchini ni takribani elfu sita na kati ya hao asilimia tisini tayari wazazi na walezi wao wanatambulika hivyo kazi iliyopo ni kutafuta namna bora ya kuwaunganisha watoto hao na familia zao.

Wadau wa mashirika pamoja na wataalam wa ustawi wa jamii wanakutana jijini mwanza ili kukubaliana na kuja na mpango mkakati utakaowezesha utekelezji kwa vitendo namnan bora ya kuondokana na tatizo la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.

Post a Comment

5 Comments

 1. Hii kwa hakika ni hatua nzuri sana. Hongera Mkuu wa mkoa kwa kuliona na kutaka au kuwa na shauku ya kulishughulikia. Niwaombe wadau mbali mbali wa watoto wafanye pia uchunguzi wa kina wa nini kinacho wakimbiza hao watoto kutoka katika familiya zao ili waweze kulitibu tatizo hilo.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Asante sana mdau wangu na ninashukusana kwa kuniandikia ujumbe huu, na hii inaonyesha kwamba unafuatilia taarifa zetu kila tunapo chapisha.

   Delete
 2. Hongera pia kwako John kabambala kwa kutujuza taarifa hiyo sisi wadau na wasio wadau wa watoto

  ReplyDelete
  Replies
  1. Zaidisana niwashukuru ninyi wote wasomaji wetu pitia tovuti hii kusoma taarifa zinazo wahusu watoto, naomba tushirikiane kuileta pamoja jamii yetu.

   Delete
 3. Zaidi sana na washukuru ninyi wasomaji wangu na watembeleaji wa tovuti yetu, endelea kutembelea ilikupata taarifa mbalimbali zinazo wahusu watoto.

  ReplyDelete