Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

ELIMU JUMUISHI ITAZAME HAKI YA WATOTO WENYE ULEMAVU WA MIGUU NCHINI.
Utekelezaji wa Elimu Jumushi katika kata ya Butelankuzi wilaya ya Bukoba, mkoani Kagera bado ina changamoto hasa Shule ya msingi Nyabushozi ambayo mazingira yake si rafiki kwa watoto wenye ulemavu wa viungo.
SILIVIA AMANDIUS ni mwandishi wa habari za watoto kutoka TKT/UN RADIO ametembelea nyumbani  kwa ASHRAFU YASINI ambaye ni mlemavu wa miguu, pia ni mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Nyabushozi, iliyopo kata ya  Butelankuzi mkoani KAGERA.

 Licha ya ulemavu huo ASHRAFU anatembea umbali mrefu kwa takribani kilometa tano, kufuata masomo shuleni, akitumia magongo (fimbo) ili kumsaidia kutembea vizuri, ameiomba serikali kutengeneza mazingira rafiki kwa wanafunzi.
“Naomba msaada wa baiskeli, natoka nyumbani naanguka pia nachelewa shuleni..” Alisema Ashirafu.

  Licha ya changamoto hiyo ASHRAFU anasoma kupitia mpango wa serikali wa elimu jumuishi ambao huwawezesha watoto wote kusoma katika shule moja na katika mazingira ya aina moja  bila ya kuwabagua watoto wenye mahitaji maalumu, pamoja na wenye ulemavu ambapo  Mkuu wa shule ya msingi Nyabushozi ALFRED JONATHAN amesema mazingira ya shule hiyo siyo rafiki kwa watoto wenye ulemavu wa viungo.

  Pia ameeleza kuwepo kwa changamoto shuleni hapo kuwa wanafunzi wengi wenye ulemavu, hukabiriwa na masuala ya utoro kutokana na miundombinu shuleni siyo rafiki.
“miundombinu ya shule siyo rafiki kwake Ashirafu, kwani madarasa yana ngazi ndefu hawezi kupanda kwa haraka pamoja na  miundombinu ya vyoo si rafiki”. Alisema Alfred Jonathan.

 TKT/UN RADIO imezungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Nyanushozi, DAUDA KATUNZI ambaye ameelezakuwa, bodi yake ndiyo inayohusika na michakato ya maboresho ya shule, ikiwemo ujenzi wa miundombinu pamoja na kuletewa  ramani kutoka halmashauri, hivyo wao wanakuwa hawajui wala kubadilisha chochote.

  Kulingana na changamoto anazopitia ASHRAFU shuleni na nyumbani, mamayake NADHIFA YASIN amesema katika kijiji chao, dhana ya ulemavu bado inatazamwa kama mkosi na licha ya hali duni ya maisha aliyonayo lakini anaamini kupitia mpango wa Elimu jumuishi mtoto wake atafika mbali.
“kuanzia darasa la kwanza nilikuwa nampeleka kwa baiskeli shuleni lakini niliugua……mtoto wangu anateseka sana katika kuitafuta elimu, na anania ya kusoma….” Alisema Mama Ashirafu.

 Kwa mujibu wa shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, Tanzania imeridhia matamko mbalimbali ya kimataifa ambayo yamelenga kuinua elimu jumuishi shuleni, miongoni mwa matamko hayo ni tamko la Haki za Watoto, tamko la Haki za Watu wenye Ulemavu lililotolewa tangu mwaka wa 1974.
Katika mahojiano ya TKT/UN RADIO, Watunga sera na Wasiamizi wa elimu katika kata ya Butelankuzi na Halamshauri ya Bukoba wamekiri kuwepo kwa changamoto na kubainisha kuwepo kwa baadhi ya viongozi wasiotekeleza maelekezo ya serikali katika uboreshaji wa sera husika.
Diwani wa kata ya Butelankuzi, GASPAL MASHONGOLE amesema wanafunzi wanapaswa kupewa fursa sawa ya elimu na kutengenezewa miundombinu bora kwa ajili ya mahitaji maalumu hasa watoto wenye ulemavu.
Hata hivyo Mwanasheria wa kujitegemea JOVIN RUTAINULWA amesema kwamba, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezungumzia haki za binadamu ikieleza haki ya mtu kutobaguliwa kwa hali yake ya kimaumbile, rangi au kabila lake.
“Serikali inapaswa kujenga mazingira mazuri ambayo yatawasaidia watoto kupata huduma kulinga na hali yao kwa watu wenye ulemavu na wasiona ulemavu” alisema Jovin
Hata hivyo Elimu Jumuishi kwa Maendeleo ya Elimu kwa Wote Tanzania, imejengwa katika msingi wa haki za binadamu, yaani kila binadamu ana haki ya kujumuika na kupata mahitaji yake kamilifu akiwa ndani ya jamii bila kutengwa wala kubaguliwa.

       Na; Silivia Amandius,  Kagera.

Post a Comment

2 Comments