Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imenyooshewa kidole baada ya kushuka kiufalu asilimia 88.13 mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 87.74 mwaka 2019.Wenyeviti pamoja na wawakilishi wa  Kamati  za Shule za Msingi za Serikali Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wamekutana na Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya kujadili mwenendo wa utoaji wa Taaluma na changamoto zake.

Akizungumza na Waandishi wa habari mgeni rasmi katika mkutano huo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, amesema majadiliano yatokanayo na kikao ndio yatakuwa maamuzi ya moja kwa moja kwa ajili ya maendeleo ya elimu katika Manispaa ya Morogoro.

Kihanga, amesema Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ilikuwa kinara  kwa miaka yote katika matokeo ya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi lakini ilipofika mwaka 2017 hali ya matokeo ilianza kubadilika kwa kuwa nyuma ya Halmashauri za Ulanga na Malinyi.

Amesema kuwa ufaulu ulikuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka isipokuwa mwaka 2019 ulishuka kutoka asilimia 88.13 mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 87.74 mwaka 2019.
“miongoni mwa sababu zilizosababisha  kushuka kwa ufaulu ni pamoja na Ongezeko kubwa la uandikishaji wa Wanafunzi kufuatia utekelezaji wa dhana ya Elimu  bila malipo  ambapo ongezeko hilo halijaenda sambamba na idadi ya miundombinu ya madarasa iliyopo pamoja na kukosekana mitihani ya mara kwa mara ya majaribio ambapo hapo awali ilikuwa ikidhaminiwa na michango ya wazazi kabla ya kuanza kwa elimu msingi bila malipo” amesema.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Michael Waluse, amesema yale yote waliyoyajadili katika kikao hicho watakwenda kuyafanyia kazi.
Amesema lengo la kukutana ni kuona ni kwa namna gani Kamati za shule zinakwenda kushirikiana na waalimu na wazazi  ili kuboresha na kuinua viwango vya ufaulu na kupata matokeo chanya katika Manispa ya Morogoro.

"Tuanze hapa tulipo kama wenzetu wameweza sisi tunashindwaje? nafikiri hiki ni kikao halali cha maamuzi ya pamoja , haiwezekanai Manispaa yetu tushike nafasi ya tatu tushindwe na Halmashauri za pembezoni ambazo zina chanagmoto nyingi, tubadilike sasa tuendelee kushikamana na nyie mliokuja leo muwe mabalozi wa kusambaza taarifa hizi kwa wenzenu ili tupige hatua matokeo hayaridhishi tukibwetea sana tutaikosa hata hiyo nafasi ya tatu tutazidi kushuka jambo ambalo litakauwa ni aibu kwa sisi tulio mjini " Amesema Waluse
Hata hivyo Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro Abdul Buhety amesema kitendo cha wanafunzi kutoka saa 9 mchana kinapelekea wanafunzi wengi kutorudi nyumbani na matokeo yake wanaishia katikati na kufanya mambo ya ajabu.

Amesema wamechukua jitihada nyingi sana za kuhakikisha ufaulu unaongezeka lakini wapo watu wachache  ambao ni waharibifu lakini watashughulikiwa ili maendeleo ya Elimu katika Manispaa ya Morogoro yaongezeke.
"Sina hakika sana hawa wanaowashtaki walimu wakuu ni wazazi au la pengine inawezekana watoto zao wanasoma shule za kulipia au watoto wao hawana akili sasa wanataka kuwaambukiza watoto wengine, niwaombe ndugu zangu tuwekeze katika elimu tusipokubali kubadilika sisi wazazi hata watoto wetu hawawezi kubadilika, kitendo cha  kuwastaki walimu kwa vikao halali mlivyokubaliana  sio jembo jema" Amesema Buhety.

 Na; Shua Ndereka-Morogoro.


Post a Comment

0 Comments