Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

DC GAIRO AWAONYA WAZAZI KUENDEKEZA NDOA ZA UTOTONI

KUFUATIA tukio la kukamatwa kwa Mkazi wa kijiji cha Ngayaki, wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro Bi. Zawadi Kitongo kwa kosa la kukaa kikao cha Mahari ya binti yake ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza, Mkuu wa Wilaya hiyo Mheshimiwa Siriel Mchembe amewaonya wazazi wanaoendekeza ndoa za utotoni.

Mheshimiwa Siriel ameipongeza kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo, kwa kufanikisha kuzuia ndoa iliyokuwa inatarajika, kufanyika siku chache zijazo kati ya Mwanafunzi huyo kutoka shule ya sekondari Madege na Bwana Julius Mchanya wote kutoka kabila la Wakamba.

Aidha amesema kwamba, kutokana na uzoefu wa wananchi wanapofanya uhalifu hujihami hasa wanapoona gari la Polisi ama gari la Serikali ilibidi gari binafsi litumike, kufanikisha zoezi la kuwakamata wahalifu.

“ilimlazimu OCD kutumia gari binafsi la askari aliyejitolea ambaye ni CPL Revocutus Sabwoya, amabaye aliambatana na Askari wa Dawati la Jinsia Hope Tarimo, askari wengine pamoja na TAKUKURU” amesema.

Kwa Upande Mwingine Mkuu wa Wilaya Siriel Mchemba amewaagiza wazazi wa wanafunzi wote ambao hawajaripoti kidato cha kwanza wajisalimishe kwenye Ofisi za Watendaji kata na vijiji ili kueleza wanafunzi wapo wapi na baada ya siku saba watakwenda kueleza katika Kituo cha Polisi.


Na SHUA NDEREKA-Morogoro.

Post a Comment

0 Comments