Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

eliza asema ulemavu wa macho sio mwisho wa ndoto zetu kielimu


Wilaya ya Kilosa ni miongoni mwa Wilaya zinazopokea misaada kutoka  mashirika mbali mbali kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu hususani shule zenye vitengo vya watoto wenye ulemavu, lakini pamoja na hayo katika shule ya msingi Mazinyungu bado wanafunzi wasioona na wenye uoni hafifu wanakabiliwa na upungufu wa mahitaji na tiba kwa ajili ya afya zao.

Elizabeth Mponji amesema changamoto  walionayo ni matibabu ya macho yao, kwani miaka iliopita walikuwa wakienda CCBRT kw ajili ya kupima macho lakini kwasasa hakuna huduma kama hiyo na macho yanawasunbua wakati wanapo kuwa darasani.
Aidha Elizabeth ameitaka jamii kuachana na dhana ya kusema mlemavu wamacho hawezi kufika mbali kielimu"ulemavu wa macho sio mwisho wa ndoto zetu kielimu"

Akizungumza na TKT/UN Radio shuleni hapo Lucy  Joseph Mwalimu wa wanafunzi wasioona amesema changamoto kubwa ni vifaa vya kufundishia,vikiwemo  ukosefu wa mashine za kuchapia vitabu vya nukuta nundu, nakuongeza kwamba changamoto zinazo tajwa na wanafunzi ni kweli hivyo akaiomba serikali na wadau wa elimu kusaidia kundi la watu wenye ulemavu.

Afisa Elimu, Elimu maalumu halmashauri ya wilaya ya Kilosa, Julius Chideliga amesema kuna baadhi ya mashirika binafsi na wadau mbali mbali hujitokeza kwa ajili ya kutoa msaada wa matibabu kwa watoto wasioona na wenye uoni hafifu.

Nae Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Kilosa,Asajile Mwambambale anasema Serikali hutenga bajeti ya mgawanyo wa mahitaji kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu kulingana na bajeti ya mwaka husika ilikuwasaidia watoto wenye ulemavu hasa kwa walio shule za bweni.

Wilaya ya KILOSA inajumla ya shule nne za msingi zinazotoa Elimu maalumu kwa wanafunzi wenye mahitaji maaalumu ambazo ni MAZINYUNGU, KICHANGANI, KIMAMBA na DUMILA ilihali shule za Sekondari ziko mbili KILOSA SEKONDARI na MGUGU sekondari.Post a Comment

0 Comments