Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Shilingi Milioni 15.3 imetumika kunulia vifaa vya ujenzi Wilayani Missenyi kukarabati Miundombinu ya Shule.
Vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 15.3 vimetolewa na Halmashauri ya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera kupitia mapato ya ndani fedha itakayotumika katika ujenzi na kukamilisha miundombinu kwenye shule nne za Sekondari.

Akizungumza katika Hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Afisa Elimu Sekondari Wilaya Bi,Savelina Misinde amesema kuwa vifaa hivyo ni mabati 490 upande wa Shule za Msingi wakati mabati 100 kwa shule za sekondari Kagera, ambazo ni Bwanjai, Bunazi na Bugandika zilizokuwa na uhaba wa vyumba vya madarasa 6 kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza na nyumba ya walimu.

Bi Savelina ameongeza kuwa fedha iliyonunulia vifaa hivyo imetokana na mapato ya ndani ya halmashauri na kwamba miundombinu hiyo ikikamilika itachangia kwa kiasi kikubwa katika kuinua kiwango cha taaluma

Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo mkurugenzi wa Halmashauri ya Missenyi Bwana, Innocent Mkandara amesema kuwa halmashauri inakusudia kutatua changamoto ya miundombinu iliyopo kwenye baadhi ya shule za msingi na sekondari mkoani Kagera na kuitaka jamii kushirikiana na Halmashauri ili kufanikisha lengo hilo

Baadhi ya wakuu wa shule zilizopatiwa misaada hiyo akiwemo Donatus Ishengoma mkuu wa shule ya Bwanjai na Steven Kamugisha wa shule ya Bugandika licha ya kuishukuru Halmashauri kwa msaada huo, wamesema kuwa miundombinu inayojengwa itasaidia kuondoa msongamano wa wanafunzi darasani sambamba na walimu kuishi karibu na maeneo yao ya kazi na kwa pamoja yatawezesha kukua kwa taaluma.

Baadhi ya madiwani wa Halmashauri hiyo akiwemo Yusuph Amada wa kata ya Kassambya na Silivia Mwandiki wa kata ya Kyaka wamesema kuwa wananchi wamekuwa wakishiriki kikamilifu katika kufamikisha shughuli za maendeleo na kwamba wataendelea kuhamasisha jamii kushirikiana na serikali kutatua changamoto mbalimbali za kielimu.

Na Rosemary Bundallah-KageraPost a Comment

0 Comments