Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Tabia ya kurithi wajane kwa baadhi ya familia ni mateso kwa watoto


Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi ccm wilaya ya Njombe bi. Angela Mwangeni  amekemea tabia ya baadhi ya wanaume kulazimisha kurithi wajane kwani kitendo hicho kinawaathiri watoto  kutopatiwa haki zao za msingi.

Bi. Mwangeni ametoa kauli hiyo wakati wa kukabidhi msaada wa fedha shilingi laki mbili za kununulia baiskeli ya kutembelea mtoto mwenye ulemavu wa miguu na mtindio wa  ubongo Gift Asukulye Kihombo mwenye umri wa miaka 13 mkazi wa kijiji cha Lole.

Amesema tabia ya kulazimisha kurithi wajane na kunyang'anya mali za watoto imebainika katika  kata ya  Ikuna ambapo imedaiwa kuna mwanaume mmoja ni kiongozi wa chama cha mapinduzi kata ya Ikuna anajihusisha na tabia hiyo na kuahidi kusimamia ili mjane huyo asimamie  na kuwalea watoto wake mwenyewe.

Kwa upande  wake diwani wa kata  ya  Ikuna ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya  Njombe  Valentino Hongoli amesema wanawake wajane wanatakiwa kuwa makini na wanaume wanaotaka kuwarithi kwani wapo wanaowarithi kwa kufuata mali huku akipongeza wazazi wa Mtoto Gifti Kihombo mwenye ulemavu kwa kushikamana kumlea.

Afisa mtendaji wa  kata  ya  Ikuna Wilayani Njombe  Bi. Alistidia  Nazar  amekili kuwepo matukio ya unyanyasaji na ukatili kwa akina mama wajane na watoto ambapo amesema serikali za vijiji bado zinaendelea kukemea tabia za kulazimisha kurithi wajene ili kuepukana na madhara ya watoto kudhurumika mali zao.
Nao wazazi wa mtoto mwenye ulemavu  huyo aliyekabidhiwa msaada wa fedha hizo kwaajili ya kununulia baiskeli akiwemo mama yake Esteri Sambanaye na Mme wake bwana Asukulye Kihombo ambao ni wazazi wenye familia ya watoto watano wameshukuru kusaidiwa msaada huo ambao utawezesha mtoto wao kutembea kwa kutumia baiskeli.

Akizungumza na kituo hiki afisa ustawi wa Jamii Wilaya ya  Njombe Averino Chaula amepongeza wananchi kwa kushiriki kukemea tabia za kurithi wajane na kusaidia  watoto wasiyo jiweza ambapo ametaka moyo huo kuendelea hata kwa kata nyingine wilayani humo.

Jumla ya  shilingi laki mbili na tisini zimekabidhiwa kwa  wazazi hao kwaajili ya kumsaidia kupata baiskeli ya magurudumu matatu mtoto Gifti Asukulye Kihombo mwenye umri wa miaka 13 ambaye anatatizo la ulemavu wa miguu na mtindio wa ubongo aliozaliwa nao.

Post a Comment

0 Comments