Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

TAKWIMU:MAAMBUKIZI YA VVU KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO

 

Huduma za kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama

kwenda kwa mtoto (PMTCT), zimeendelea kutolewa, ambapo kwa mwaka 2019, jumla ya akina mama wajawazito 2,232,500 sawa na asilimia 98 ya akina mama 2,272,866 walipatiwa huduma za ushauri nasaha na upimaji wa VVU.

 Kati yao akina mama 34,764 sawa na asilimia 1.6 waligundulika kuwa

wanaishi na VVU. Akina mama 82,408 sawa na asilimia 91 ya akina mama wenye maambukizi ya VVU walipatiwa dawa (ARV) kwa ajili ya kufubaza virusi vya UKIMWI.

 Aidha, jumla ya Watoto 44,711 sawa na asilimia 52 walipata kipimo cha awali cha utambuzi wa maambukizi ya VVU ambapo watoto 1,128 sawa na asilimia 2.5 walikutwa na maambukizi ya VVU.

 Kiwango hicho cha maambukizi kinaashiria Tanzania ipo katika kasi sawia ya kuweza kufikia maambukizi chini ya asilimia 2 ifikapo mwaka 2021 kama inavyoainishwa katika mpango mkakati wa kutokomeza kabisa maambukizi ya VVU kwa watoto.

Chanzo:Hotuba ya Wizara ya Afya maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto ya mwaka 2019/2020.

Waandishi wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi: -

John Kabambala: kabambalajohn@gmail.com

Hamad Rashid: hamadrashidhd@gmail.com

 


Post a Comment

0 Comments