Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

TAKWIMU:WANAFUNZI WASIOTIMIZIWA KIKAMILIFU MAHITAJI YA MSINGI NYUMBANI

 

Kwa mujibu wa Ripoti ya utafiti wa Hali ya Ukatili kwa watoto Shuleni Tanzania Bara Ripoti ya mwaka 2020, kutoka Shirika la Haki Elimu Tanzania inaeleza wapo watoto walioshindwa kutimiziwa mahitaji yao ya msingi na wazazi au walezi wao ilihali walikua na uwezo huo.

Mahitaji ya msingi waliyopuuza wazazi/walezi kutimiza kwa watoto wao ni matibabu ya kiafya, chakula, malazi, mavazi, Elimu, uangalizi mzuri wa watoto nakadhalika.

Aidha wanafunzi waliohojiwa kama wazazi na walezi wao walipuuzia kuwatimizia mahitaji yao na wakajibu ndio, walisema aina ya mahitaji waliyoshindwa kutimiziwa kikamilifu ni, kutopata chakula cha kutosha na vinywaji, kuvaa nguo chafu, kuvaa nguo zilizochanika, kuvaa viatu vidogo, kutopelekwa hospitali pindi walipougua kumuona daktari au kupewa dawa lakini pia hawakua wanapatiwa malezi mazuri.

Jedwali hapo chini linafafanua idadi ya wanafunzi walioshindwa kutimiziwa mahitaji yao ya Msingi katika maeneo ya mijini, vijijini na katika Shule za Msingi na Sekondari za Binafsi na za Serikali Tanzania Bara.

JINSI

MSINGI

SEKONDARI

Wavulana

Wasichana

Jumla

Wavulana

Wasichana

Jumla

Mjini

205 (84.7%)

229 (84.2%)

434 (84.4%)

60 (27.6%)

51 (18.0%)

111 (22.2%)

Vijijini

42 (21.0%)

40 (19.5%)

82 (20.2%)

43 (24.2%)

36 (15.9%)

79 (19.5%)

Shule za Binafisi

12 (9.9%)

18 (13.0%)

30 (11.6%)

22 (19.5%)

32 (17.7%)

54 (18.4%)

Shule za Serikali

67 (20.9%)

65 (19.2%)

132 (20.0%)

81 (28.7%)

55 (16.7%)

136 (22.3%)

Jumla

79 (17.9%)

83 (17.4%)

162 (17.6%)

103 (26.1%)

87 (17.1%)

190 (21.0%)

Chanzo: HakiElimu Tanzania.

Waandishi wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: -

John Kabambala: kabambalajohn@gmail.com  

Hamad Rashid: hamadrashidhd@gmail.com  

 

Post a Comment

0 Comments