Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

TAKWIMU: WASTANI WA UFAULU SOMO LA KINGEREZA UKO CHINI KWA DARASA LA TATU HADI LA SABA

 

                                      Picha: Habari leo

Ripoti ya utafiti wa kujifunza iliyotolewa Mwaka 2019 na Shirika la Uwezo Tanzania, inaonesha idadi kubwa ya watoto wa darasa la 3 hadi la 7 bado hawana ujuzi wa msingi wa kusoma na kuhesabu. Na kiwango cha ufaulu wa somo la  Kiswahili kwenye majaribio ya wanafunzi uliongezeka kwa wanafunzi wa Darasa la 6 ambapo ufaulu ulikuwa wa 89%. 

Hata hivyo Ripoti ya Uwezo Tanzania inafafanua wastani wa ufaulu kwa Darasa la Tatu hadi Darasa la Saba kwa somo la Kingereza uko chini ukilinganisha na ufaulu wa somo la Kiswahili kwa madarasa hayo hayo, wakati huo Darasa la Tatu likifanya vibaya kutoa matokeo yenye ufaulu wa chini kabisa kuliko Darasa la Saba kwa somo la Kingereza kwanzia Mwaka 2011-2017. 

Jedwali hapo chini linaeleza zaidi kiwango cha ufaulu kwa majaribio ya Somo la Kingereza.

 

Darasa la Tatu

12%

12%

19%

21%

13%

14%

15%

Darasa la Saba

48%

53%

56%

56%

48%

47.5%

47%

Mwaka

2011

2012

2013

2014

2015

2016

2017

Chanzo: Uwezo Tanzania.

Waandishi wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: -

John Kabambala: kabambalajohn@gmail.com  

Hamad Rashid: hamadrashidhd@gmail.com  

 

Post a Comment

0 Comments