Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

TAKWIMU: ZA UFAULU SOMO LA KISWAHILI KWA SHULE ZA MSINGI.

 

Katika muendelezo wa uchambuzi wa Takwimu mbalimbali hatimaye tumeanza kuangazia Ripoti ya Tathmini ya Kujifunza kwa wanafunzi wa Shule za Msingi kutoka Shirika la Uwezo Tanzania iliyofanyiwa utafiti kipindi cha Miaka sita ikikamilika 2017 na kutolewa Mwaka 2019.

 Ripoti hiyo ilihusisha jumla ya Kaya 276,992 na watoto waliwafanyiwa utafiti ni 614,733 Katika kipindi cha miaka sita kuanzia Mwaka 2011, 2012, 2013, 2014, 2015, na 2017.

 Aidha kwa Mwaka 2017 pekee, utafiti wa Uwezo Tanzania ulizifikia Kaya 25,532 na watoto 64,639 na mwaka ulioongoza kuwafikia watoto wengi zaidi na Kaya nyingi ni 2015 ambapo jumla ya watoto 197,451 walifikia na Kaya 68,588.

 Tukibaki katika Mwaka 2017 Ripoti ya utafiti wa kujifunza inaonesha, idadi kubwa ya watoto wa darasa la 3 hadi la 7 bado hawana ujuzi wa msingi wa kusoma na kuhesabu. Na kiwango cha ufaulu wa somo la  Kiswahili kwenye majaribio ya wanafunzi uliongezeka kwa wanafunzi wa Darasa la 6 ambapo ufaulu ulikuwa wa 89%.

 Wastani wa ufaulu kwa Darasa la Tatu ulikua ni 70% Darasa la nne ni 80% la Tano ni 88% na Darasa la Saba ni 86% .

 Jedwali hapo chini linaeleza zaidi kiwango cha ufaulu kwa majaribio ya Somo la Kiswahili. 

 

MWAKA

 

DARASA

KIWANGO     CHA UFAULU

 

SOMO

 

 

2017

III

70%

KISWAHILI

IV

80%

KISWAHILI

V

88%

KISWAHILI

VI

89%

KISWAHILI

VII

86%

KISWAHILI

Chanzo: Uwezo Tanzania.
Waandishi wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: -
John Kabambala: kabambalajohn@gmail.com  
Hamad Rashid: hamadrashidhd@gmail.com  

 

Post a Comment

0 Comments