Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

VITUO VILIVYOKIDHI KUFANYA HUDUMA YA UPASUAJI WA KUMTOA MTOTO TUMBONI.

Mwaka 2020, idadi ya vituo vilivyo karabatiwa kwa ajili ya kutoa huduma ya upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni iliongezeka na kufikia 487 mwaka 2020 kutoka vituo 352 mwaka 2019, sawa na ongezeko la asilimia 38.4, Kwa mujibu wa ripoti ya kitabu cha hali ya uchumi wa taifa katika mwaka 2020.

Ongezeko la vituo hivyo vya Afya ilichangiwa na jitihada za Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta binafsi kuendelea kuboresha miundombinu ya afya.

Aidha, idadi ya vituo vya kutolea huduma za uchunguzi wa mabadiliko ya awali ya Saratani iliongezeka na kufikia vituo 746 mwaka 2020 kutoka vituo 624 Mwaka 2019, ambapo wanawake 533,780 walifanyiwa uchunguzi ikilinganishwa wanawake 413,851waliofanyiwa uchunguzi Mwaka 2019.

Chanzo: Wizara ya Fedha na Mipango.

Waandishi wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: -

John Kabambala: kabambalajohn@gmail.com 

Hamad Rashid: hamadrashidhd@gmail.com

Post a Comment

0 Comments