Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

WATOTO MILIONI 9 WALIPATIWA MATONE YA VITAMINI ‘’A’’ HADI KUFIKIA 2020

 

                                                     Picha na Ipp media

Kwa mujibu wa ripoti ya kitabu cha hali ya uchumi wa taifa katika mwaka 2020 kutoka Wizara ya Fedha na mipango, katika ukurasa wa 260 kipengele cha Lishe, kinaeleza kuwa Mwaka 2020, Serikali iliendelea kutekeleza Mpango Jumuishi wa Taifa wa Lishe wa (2016/17 - 2020/21) ili kukabiliana na athari za lishe duni na kuimarisha ukuaji mzuri wa mwili na akili kwa mtoto.

Katika kipindi hicho cha Mwaka 2020/2021, zaidi ya asilimia 90% ya watoto milioni 9 walio chini ya umri wa miaka mitano walipatiwa matone ya Vitamini A.

Aidha, asilimia 91.3% ya watoto waliozaliwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya Mwaka 2020 walinyonyeshwa ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa ikilinganishwa na asilimia 89.9% walionyonyeshwa mwaka 2019. Vile vile, asilimia 5.6% ya watoto walizaliwa na uzito pungufu mwaka 2020 ikilinganishwa na asilimia 5.7% ya watoto Mwaka 2019.

Kwa upande mwingine, asilimia 0.9% ya wajawazito waliopimwa wingi wa damu katika hudhurio la kwanza walikuwa na upungufu mkubwa wa damu ikilinganishwa na asilimia 1.4% ya Mwaka 2019. 

Chanzo: Wizara ya Fedha na Mipango.

Waandishi wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: -

John Kabambala: kabambalajohn@gmail.com 

Hamad Rashid: hamadrashidhd@gmail.com

Post a Comment

0 Comments