Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

JAMII IMEKUMBUSHWA KUWAJALI WANAWAKE WAJANE NA KUWAPA MSAADA WANAPOHITAJIJamii imekumbushwa kuona umuhimu wa kuwajali wanawake wajane ambao mara kadhaa wamekua wakikosa msaada katika familia zao baada ya kufiwa na waume wao ili na wao waishi maisha ya furaha sawa na wengine.

Mwishoni mwa Mwaka 2021 Mwezi Disemba Tanzania kids time ilihudhuria Mkutano wa wanawake wajane 130, waliopewa mafunzo Mkoani Morogoro wakifundishwa jinsi ya kuishi maisha baada ya kufiwa na waume wao.

Ikiwa ni Mwaka wa Tisa tukio hili linafanyika, ambapo Mwaka 2021 lilifanyika ndani ya Ukumbi wa wa Mikutano wa La Miriam uliyopo Mjini Morogoro, wajane 130 wamehudhuria mafunzo ya siku Saba wakipewa Elimu ya nama ya kuishi maisha baada ya kufiwa ikiwemo kujitahidi kujali Afya zao, matumizi ya vyakuala asilia, kuwa na upendo pamoja na kujishughulisha na kazi mbalimbali za kujipatia kipato.

Mafundisho waliyopata wajane yaliwapa faraja na kujiona kuwa ni Jasiri na sio wanyonge tena, walisimulia Amina Mbwana Mjane kutoka Kisalawe, Pwani na Edith Chitukuro Mjane kutoka Jiji la Dodoma ,walipohojiwa na Tanzania Kids Time.

Amina Mbwana alisema “tumekutanishwa hapa kututoa ule msongo wa mawazo kwamba kufika ni balaa lakini kumbe kufiwa ni jambo la kawaida, watu walikua wanakaa wakilia, kumbe hutakiwi kulia inabidi umwamini Mungu na kusonga mbele”

Mkutano huu umeweza kututia faraja kwa yale mafunzo ambayo tumeweza kupewa, tumeambiwa wajane sio watu wa kulia, ndio jambo ambalo nimejifunza” alisema Edith Chitukuro Mjane kutoka Mkoa wa Dodoma.

Miongoni mwa wawezeshaji wa Mafunzo katika Semina hiyo ya wajane ni Mjane na mwanasheria mstaafu Ester Mtaki kutoka Mkoa wa Mwanza na Tabibu wa magonjwa ya Binadamu David Lugomela Mkazi wa Morogoro, kwa pamoja walijikita kuwafundisha wajane kujali Afya ya Macho pamoja na kutokalia haki zao badala yake wawe wakifuata Sheria kupata Haki zao.

Mhutubu mkuu wa Mkutano Simbarashe Charumbira kutoka nchini Canada nae alieleza changamoto zinazowasumbua wanawake wajane ikiwemo kukosa kushughulisha akili wakiamini wao ni watu wa kusaidiwa kila siku.

“Tumekua hapa kwa ajili ya mkutano huu wa wajane tumejifunza mengi na nitumie fursa hii kuwahamasiha wajane wengine walioko Nyumbani wakati mwingine waweze kushiriki, nilichokiona kwa wajane hawapendi kutumia akili zao lakini pia tumewafundisha vitu vya kufanya Nyumbani kwao ili kuimarisha Afya zao ili waishi maisha mazuri” alisema Simbarashe Charumbira

Neema Tuvako ndiye mratibu wa Semina hii iliyopewa jina la Muendelezo wa maisha ya wajane.

“lengo langu kabisa ifike mahali Jamii ione umuhimu wa kujali wajane wao, kwasababu kwakweli anayemtesa Mjane sio Mtu wa mbali, ni Mtu wa Jamii, ni Mtu wa Familia kwa hiyo Jamii ifike mahali ithamini wajane wao, ithamini wale watoto, sisi tunaamini kwamba ukimsaidia mjane mmoja naye anaweza kusaidia Yatima wake” alisema Neema Tuvako.

 

Post a Comment

0 Comments